Rais
wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Dkt. John Magufuli amemteua Prof
Andrew Barnabas Pembe kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi
Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Taarifa
iliyotolewa na Katibu Mkuu kiongozi, Balozi John Kijazi kupitia
Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa imesema kuwa uteuzi wa
Prof. Pembe umeanza siku ya leo.
Kabla
ya uteuzi huo Prof. Pembe alikuwa Mhadhiri na Kaimu Makamu Mkuu wa
Chuo hicho anayeshughulikia taaluma, utafiti na ushauri.
0 comments:
Chapisha Maoni