Baadhi
ya wabunge wamemshauri Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
kuchukua hatua mbalimbali ili kutatua migogoro ya ardhi nchini.
Wabunge hao wameyasema hayo leo bungeni jijini Dodoma walipokuwa wakichangia bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2018/19
Mmoja
wa wabunge waliochangia wizara hiyo ni Mbunge wa Kuteuliwa na Rais,
Anne Kilango (CCM), ambaye amesema mashamba ya mkonge yaliyoko katika
Kata za Makanya na Ndungu wilayani Same Mkoa wa Kilimanjaro, hayana
faida kwa wananchi wa kata hizo.
“Kutokana
na hali hiyo naiomba Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
ichukue hatua ili kuwapa ardhi vijana na wananchi wa kata hizo,”.
Wakati
huo huo, Mbunge wa Liwale, Zuberi Kuchauka (CUF) aliitaka wizara hiyo
iongeze kasi ya kutatua migogoro kwa kuwa inarudisha nyuma maendeleo ya
wananchi.
Kwa
upande wake Mbunge wa Tabora Mjini, Emmanuel Mwakasaka (CCM) aliitaka
serikali ifanye uhakiki wa viwanja vyote vyenye migogoro ili kujua
wamiliki halali wa maeneo hayo.
0 comments:
Chapisha Maoni