Wabunge
wa Chadema leo Jumatano Mei 30, 2018 hawajahudhuria kikao cha Bunge la
Bajeti, kwa madai kuwa wengi wamekwenda mkoani Kigoma kushiriki maziko
ya aliyekuwa mbunge wa chama hicho, Kasuku Bilago.
Bilago
ambaye alikuwa mbunge wa Buyungu, alifariki dunia Jumamosi Mei 26, 2018
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Aliagwa jana na wabunge
kwenye viwanja vya Bunge na mwili wake kusafirishwa mkoani Kigoma kwa
maziko.
Eneo
wanaloketi wabunge wa chama hicho ndani ya ukumbi wa Bunge, lipo tupu,
wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo asubuhi, maswali ya wabunge
hao wa Chadema likiwamo la Joseph Mkundi (Ukerewe), yaliulizwa na
wabunge wa CCM.
0 comments:
Chapisha Maoni