Mbunge
wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu Sugu (Chadema), ameliambia
Bunge kuwa wakati akiwa gerezani, alipokea salamu kutoka kwa viongozi na
wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) huku akimpongeza Prof. Mark
Mwandosya kwa kuwa mwana CCM pekee aliyekwenda kumsalimia gerezani.
Akichangia
bungeni jijini Dodoma jana mjadala wa makadirio ya Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa mwaka ujao wa fedha, Sugu
aliwapongeza viongozi na wabunge wa CCM kwa kumtumia salamu gerezani
huku akidai wengi wao waliogopa kwenda kumjulia hali.
Hata
hivyo, Sugu alisema CCM waliwakilishwa vizuri na waziri wa zamani Prof.
Mwandosya ambaye ndiye pekee wa chama tawala hicho aliyefika gerezani
kumjulia hali.
Mbunge
huyo ambaye jana alikuwa wa kwanza kuchangia mjadala huo, pia alitumia
fursa hiyo kutoa pole kwa wananchi wa Mbeya ambao alidai waliungana naye
kutumikia kifungo hicho.
"Nawashukuru
watu wote waliopaza zauti zao kulaani kifungo dhidi yangu," alisema
Sugu katika maneno yake ya utangulizi kabla ya kujikita katika hoja
iliyokuwa bungeni.
Mbunge
huyo mwanzoni mwa mwaka huu alihukumiwa kifungo cha miezi mitano
gerezani baada ya kukutwa na hatia kisha kuachiwa wiki mbili zilizopita
kwa msamaha wa Rais.
Katika
mchango wake jana, Sugu alisema matukio ya uhalifu na vifungo dhidi ya
wanasiasa kama yeye yanayotokea nchini yanawafanya baadhi ya wawekezaji
kuogopa kuja kuwekeza nchini.
Alisema
pamoja na kwamba Tanzania inaweza kuwa na jitihada za kuwashawishi
wawekezaji kutoka nje kuwekeza nchini, mkakati huo huenda usifanikiwe
kwa kuwa wawekezaji wanapenda kuwekeza katika nchi zenye usalama kuliko
nchi zenye vurugu na mauaji.
Sugu
pia alimshauri Rais aanze kusafiri kwenda nje ya nchi akisisitiza kuwa
safari za nje zina faida kama ilivyokuwa enzi za uongozi wa Rais mstaafu
Jakaya Kikwete aliyekuwa akisafiri mara kwa mara.
“Pamoja
na hayo, serikali haiwatendei haki Watanzania wanaoacha kazi nje na
kuja kufanya kazi nchini kwa sababu inataka iwalipe mishahara midogo
kama ilivyotokea kwa bosi mmoja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),"
Sugu alisema.
0 comments:
Chapisha Maoni