Mbunge
wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma Kasheku, amefungukia madai
yaliyowahi kutolewa na Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe, kwamba
walitekwa na watu wa usalama wa Taifa ni ya uongo na kwamba kilichotokea
walikamatwa na askari na mbinu zilizotumika ni zile wanazofundishwa
bungeni.
Musukuma
ametoa kauli hiyo jana wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha
Kikaangoni kinachorushwa na EATV , ambapo alifafanua kwamba walikuwa
wakidhaniwa kufanya uhalifu.
Musukuma
alisema kwamba "Mara ya kwanza kulala polisi nimelala nikiwa mwana-
CCM, mara ya kwanza Dodoma, mara ya pili ni Geita, na nilikubali kwa
sababu wala hatukutekwa, nilikuwa na kina Bashe, nilimsikia rafiki yangu
Hussein Bashe alisema tumetekwa, hatukutekwa".
"Tulikamatwa
tukapelekwa polisi, tukapekuliwa, tulipoonekana hatuna hatia tukaachiwa
, hatukutekwa. Sikumjibu Hussein Bashe aliposema tumetekwa kwa sababu
sikuwepo, nasema hapa hatukutekwa," Musukuma.
Aprili
11, 2017 Mbunge wa Nzega Mjini(CCM) Hussein Bashe aliwataka wabunge
kuacha unafiki kuhusu Usalama kuwateka watu na kwamba yeye ni mmoja wa
watu waliokamatwa wakati wa mkutano Mkuu wa CCM.
"Mimi
nimekamatwa na kuteswa na Usalama wa Taifa. Nimenyanyaswa sana nchi
hii. Ikibidi mnifukuze CCM - " alisema Bashe wakati Waziri wa
Tamisemi,(kabla hajaenguliwa katika nafasi hiyo) George Simbachawene
kumtaka Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kuthibitisha kuwa matukio ya
ukamataji yanafanywa na usalama wa Taifa.
0 comments:
Chapisha Maoni