Mashindano hayo yatafanyika Nairobi Kenya ambapo mshindi wa mashindano hayo atakwenda England kucheza na moja ya timu ambazo zinadhaminiwa na kampuni hiyo.
Kwa upande wa Tanzania timu zitakazoshiriki michuano hiyo inayotarajiwa kuanza mapema mwezi Juni 2018 ni Yanga, Simba, Singida United pamoja na JKU ya Zanzibar.
“Mashindano hayo yalianza hapa (Tanzania) mwaka jana na sasa yanakwenda Kenya kwa mtazamo uleule na mafanikio yaleyale yaliyopatikana mwaka jana lakini safari hii mafanikio yatakuwa makubwa sana kwa sababu mshindi wa mashindano haya anaweza kwenda kucheza Uingereza”-Abbas Tarimba, mwakilishi wa SportPesa Tanzania.
“Mshindi atakaekwenda kucheza Uingereza atanufaika si tu na dakika 90 za mchezo lakini kuna mambo mengi ambayo wanaweza kujifunza ikiwa ni pamoja na kuendeleza weledi wao katika mpira wa miguu.”
“Mashindano yatashirikisha timu nane, nne kutoka Kenya na nne kutoka Tanzania hivyo ni mashindano yenye chachu kubwa sana na yanafanyika wakati mzuri sana.”
0 comments:
Chapisha Maoni