Anafahamika zaidi kama Rose Ndauka ni mmoja warembo wenye mvuto wa pekee ndani ya tasnia ya bongo movies kwa vipaji vyake vingi sana.
Licha
ya kuwa na uwezo mkubwa wa kuigiza pia ose ni mwandishi na mwongozaji
wa Filamu.
Akiwa ameshaigiza kwenye zaidi ya Filamu kumi na saba (17) na
kupata tuzo mbalimbali ikiwemo ya best actress in mini ziff 2011; Rose
Pia ni mfanyabishara na anamiliki kampuni yake binafsi iitwayo Ndauka
Entertainment inayojihusha na mambo ya Filamu na burudani.
Rose Hupenda
kusikiliza muziki, kuogelea, na kusoma vitabu akiwa yupo nyumbani
Historia ya Rose inaanza tarehe saba (7) mwezi wa kumi (10) mwaka
1989. Huu ni mwaka tarehe na siku alipozaliwa.
Alizaliwa hapa hapa Tanzania na kupata elimu yake katika shule ya sekondari zanaki- Dar es salaam . Toka alipokuwa mdogo sana Rose alipenda kuigiza.
Alizaliwa hapa hapa Tanzania na kupata elimu yake katika shule ya sekondari zanaki- Dar es salaam . Toka alipokuwa mdogo sana Rose alipenda kuigiza.
Kipaji chake Kiligunduliwa na mama yake mzazi kabla
ya yeye mwenyewe kuamua kujiingiza rasmi kwenye tasnia ya Filamu
nchini.
Rose alionekana kwa mara ya kwanza kwenye Filamu ya “SWAHIBA”
aliyoigiza kama “Aisha” mnamo mwaka 2007. Filamu hii ilipigiwa kura kama
Filamu bora ya mwaka na kituo cha redio cha clouds FM.
Baada ya Filamu
hiyo Rose aliweza kupata nafasi ya kuigiza katika Filamu mbalimbali
zikiwemo Mahabuba na Solemba na nyota yake ilionekana sana pale
alipoigiza Filamu ya Deception na marehemu Steven Kanumba kama mmoja wa
waigizaji wakuu pamoja na Lost Adam aliyoigiza na mkali mwingine wa
bongo movies Jacob steven “JB”
Mwaka 2010 Rose Ndauka alifungua kampuni yake mwenyewe ya
“Ndauka Entertainment” na pia alipata nafasi ya kuigiza kwenye Filamu
inayohusu mauaji ya halaiki ya Rwanda iliyopewa jina la “RWANDA BAADA YA
VITA” ama (URWANDA NYUMA U’GENOCIDE) kwa kirwanda.
Mwaka huo huo chini ya kampuni yake Rose alitoa filamu mbili za “BAD GIRL” na “THE DIARY” ambazo zilifanya vizuri sana sokoni.
Mashabiki wake wanapenda kuita “Rosie” na mara nyingi amekuwa
akipata “attention” kubwa kwenye vyombo vya habari na magazeti kutokana
na mvuto wake na umbo lake zuri.
0 comments:
Chapisha Maoni