Ofisa
Utumishi Mkuu Wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Evans Emil ameieleza Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Ofisa Msaidizi wa Forodha wa TRA Jennifer
Mushi anayedaiwa kumiliki magari 19 yasiyolingana na kipato chake
anamiliki baadhi ya mali asilimia 50 kwa 50 na familia yake.
Emil
ambaye ni shahidi wa kwanza katika kesi hiyo ameyaeleza hayo wakati
akijibu maswali ya wakili wa serikali Pius Hilla mbele ya Hakimu Mkazi
Mkuu Wilbard Mashauri.
Katika
ushahidi huo Emil amedai kuwa July Mosi, 2011 Jennifer alipewa ajira na
kupatiwa fomu mbalimbali ajaze ikiwamo fomu ya Tamko ya Rasilimali na
madeni. Katika fomu hiyo ya rasilimali March 30,2012 imeonyesha Jennifer
anamiliki fedha taslimu Sh.Laki 6 zilizopo katika benki na taasisi za
fedha Sh 800,000.
Pia
alikuwa na Hisa na gawio la thamani ya Sh.Laki 6, anamiliki nyumba
Kinyerezi Kichangani ya Sh.Mil 30 ambapo anamiliki asilimia 50 kwa 50
baina yake na mumewe, vilevile anamiliki shamba la Heka 1 Mabwepande
lenye thamani ya Sh.Laki 7, ambapo anamiliki asilimia 50 kwa 50 baina
yake na mumewe.
Pia
anamiliki Kiwanja Heka 1 Kigamboni thamani yake ni Sh.Mil 9 ambapo
umiliki wake wake asilimia 50 kwa 50 na mumewe Pia anamiliki gari aina
ya Van T 884 BNU thamani Sh.Mil 8 umiliki wake asilimia 50 na mume
asilimia 50.
Katika
fomu ya tamko ya rasilimali na madeni ya February 20, 2013 alikuwa na
fedha taslimu Sh. Laki 8 pamoja fedha zilizopo taasisi za fedha ni
Sh.Mil 1, nyumba Kinyerezi thamani ya Sh.Mil 35 ambapo umiliki wake ni
asilimia 50 kwa 50 na mumewe.
Pia
anamiliki Kiwanja eneo la Bunju thamani ya Sh.Mil 1.7, pia kiwanja
kilichopo Kigamboni thamani ya Sh.Mil 9 ambacho wanamiliki ni watoto
wake.
Pia
ana magari mawili aina ya RV4 moja ikiwa na thamani ya Sh.mil 8 na
jingine Sh.Mil 13 ambapo umiliki wake asilimia 50 kwa 50 na mumewe.
Katika
fomu ya tamko ya rasilimari na madeni ya December 11,2015 inaonyesha
ana fedha taslimu benki Sh. Laki 5 na katika taasisi za fedha Sh.Mil
2.7, Pia ana kiwanja Kigamboni cha Sh.Mil 9 ambapo umiliki wake wake ni
asilimia 50 kwa 50 na mumewe.
Pia
ana magari mawili aina ya Toyota moja ni Sh.Mil 18 na jingine Sh.Mil
14.Pia ana Deni la saccos ya TRA la Sh.Laki 6. Baada ya kueleza hayo,
Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi June 6,2018 ili kuendelea na
shahidi wa pili.
Katika
kesi hiyo mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa kati ya March 21,2016 na Juni
30,2016 jijini Dar es Salaam akiwa mwajiriwa wa TRA kama Afisa Forodha
Msaidizi alikutwa akimili magari 19 yenye thamani ya Mil.197 kinyume na
kipato chake halali. Pia amekutwa akiishi maisha ya kifahari yenye
thamani ya Sh.Mil 333 fedha ambayo hailingani na Kipato chake halali.
0 comments:
Chapisha Maoni