Mahakama
Kuu ya Mtwara imeondoa mahakamani shauri la kupinga matumizi ya Kanuni
za Maudhui ya Kimtandao (Online Content Regulation) lililofunguliwa na
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na wenzake dhidi ya Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Mbali
na LHRC wengine waliopeleka zuio hilo ni Tanzania Human Rights
Defenders (THRD); Baraza la Habari Tanzania(MCT) na Jamii Media; Chama
cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa ); na Jukwaa la
Wahariri (TEF).
Kanuni
hizo zilipaswa zianze kutumika Mei 5 lakini mahakama hiyo ikaweka zuio
la muda Mei 4, baada ya kuwasilishwa kwa shauri la kupinga mahakamani
hapo.
Kesi
hiyo namba 12/2018 ilisomwa jana Mei 28 mbele ya Jaji Mfawidhi, Dk Fauz
Twaib na ilipangwa kutolewa uamuzi juu ya mapingamizi matatu
yaliyowasilishwa na upande wa Serikali.
Akitoa
uamuzi huo jana, Jaji Dk Twaib alisema mahakama hiyo imekubali
pingamizi moja kati ya matatu yaliyowasilishwa; kwamba mashirika
yaliyopeleka kesi mahakamani hapo hayana maslahi ya kutosha kwa maana ya
kufungua shauri hilo na kwamba hawakuonyesha namna moja kwa moja
yatakavyoguswa na kanuni hizo.
Hivyo,
mahakama iliondoa shauri hilo lakini inatoa nafasi kwa mashirika hayo
kama yatahitaji kupeleka shauri lingine kama watajidhihirisha wana
nafasi ya kufanya hivyo.
Credit: Mwananchi
0 comments:
Chapisha Maoni