Siku
ya Walinda Amani Duniani huadhimishwa tarehe 29 Mei ya kila mwaka
ambapo kaulimbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni “Ulinzi wa Amani
wa Umoja wa Mataifa: Miaka 70 ya huduma na kujitoa (UN Peacekeeping: 70
Years of Service and Sacrifice).
Katika
hotuba yake, Mhe. Waziri Mahiga alieleza kuwa yapata miaka 12 tangu
Tanzania ianze kushiriki katika ulinzi wa amani chini ya bendera ya
Umoja wa Mataifa.
Pia
akasisitiza Tanzania itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha
inasaidia kupatikana kwa amani katika mataifa mengine kwakuwa hakuna
taifa linaloweza kufanikiwa katika maendeleo pasipo kuwepo na amani ya
uhakika.
"Sio jambo rahisi kukubali kutoa uhai wako kwa ajili ya mtu mwingine lakini Tanzania itaendelea kuungana na mataifa mengine duniani katika kusaidia kupatikana kwa amani ya mataifa hayo" alisema Mhe. Mahiga.
"Sio jambo rahisi kukubali kutoa uhai wako kwa ajili ya mtu mwingine lakini Tanzania itaendelea kuungana na mataifa mengine duniani katika kusaidia kupatikana kwa amani ya mataifa hayo" alisema Mhe. Mahiga.
Aidha,
Katika kuwakumbuka Walinda Amani wote Duniani waliopoteza maisha wakati
wakitekeleza majukumu yao, pamoja na kutoa heshima kwa wale ambao bado
wanaendelea na jukumu la kulinda amani, Tanzania imepoteza jumla ya
askari wapatao 30 ndani ya miaka 10, pia dunia imepoteza zaidi ya askari
3500 na kwa sasa Tanzania inajivunia kuwa na jumla ya askari wapatao
2,600 wanaohudumu katika misheni sita (6) za ulinzi wa Amani za Umoja wa
Mataifa.
0 comments:
Chapisha Maoni