Msanii
mkongwe wa taaarabu nchini Khadija Kopa amefunguka na kuzungumzia hali
ya taarabu ilivyo sasa nchini na kusema kuwa wasanii wengi wamekuwa
jeuri na kwamba hawajitunzi kama zamani hivyio wanajishusha thamani wao
wenyewe na wala sio kitu kingine.
Khadija
kopa anasema kuwa wasanii wa taarabu wamekuwa wakiimba katika ma bar
kwa kiinglio cha bia wakati hiyo haikuwa kama zamani na ili kukomesha
hilo waimbaji hao wanatakiwa wakifuatwa wasikubali kufanya hivyo na
kujiona wa thamani ili kupanda hadhi yao.
Hata
hivyo akizungumzia swala la yeye kustaafu kama alivyofanya gwiji wa
taarabu nchini, mzee Yusup, malkia huyo amesema kuwa alichokifanya mzee
ni kutokana na imani yake ilivyomtuma na ni jambo zuri , hata yeye siku
yoyote atastaafu na sio muda mrefu kutoka sasa kwa sababu anahitaji
kutenga muda mwingi pia kwa ajili yake , dini na mungu wake kwa sababu
hajuai siku wala saa ya kufa kwake.
Hata
hivyo Khadija Kopa anasema kuwa kama ataamua kufanya hivyo atafanya
kimya kimya bila kumwambia wala kutangaza kwa watu, bali watashangaa tu
haingii tena studio wala haonekani tena katika maswala ya burudani.
"Sina
muda mrefu sana nitaacha huu muziki na nitakapo acha wala sina haja ya
kutangaza eti eeh ninaacha muziki, hapana nitaacha tu na watu wataona
kimya tu sitoi nyimbo."
0 comments:
Chapisha Maoni