Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Polisi Tarime Rorya Henry Mwaibambe amethibitisha
kuuawa kwa Bwana Chacha Heche Suguta ambaye ni mdogo wa Mbunge wa Tarime
Vijijini John Heche, kwa kuchomwa kisu na Polisi.
Kamanda
Mwaibambe amesema marehemu alikuwa na mgogoro na mmoja ya askari
waliokuwa wamemkamata, na kufikia hatua ya kutaka kushikana (kupigana)
ndipo askari aliposhindwa kujizuia na kumchoma kisu.
“Tukio
ni la kweli limetokea na huyo askari tunamshikilia, huyo kijana
alikamatwa usiku sasa wakati wapo kwenye gari wakielekea kituo cha
polisi, ukatokea mzozo kati ya huyu askari na huyu marehemu, mzozo kama
wanataka kupigana, mwenzake akaingilia kuamua, lakini ni kweli askari
amemjeruhi huyu mgongoni, mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi leo saa
6 mbele ya ndugu zake, kweli umekutwa na jeraha la hicho kisu mgongoni
na mtuhumiwa alikuwa hajavalishwa pingu, ila hatujui nini waliambiana
mpaka kufikia hivyo”, amesema Kamanda Mwaibambe.
Sambamba
na hilo Kamanda Mwaibambe amesema hali ya kituoni hapo kwa sasa
imetulia baada ya wananchi kufurika kulalamikia mauaji hayo, na kwamba
amezungumza na ndugu wa familia kuwaeleza jinsi tukio lilivyokuwa.
Pia
Kamanda Mwaibambe amewataka watu kutochukulia tukio hilo kisiasa,
isipokuwa ni kama tukio lingine la mauaji, ingawa sio jambo zuri kwa mtu
yeyote.
0 comments:
Chapisha Maoni