Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe ameripoti Kituo Kikuu cha Polisi saa nane mchana na kuondoka saa 8.20 mchana.
Vingozi
wengine walioripoti ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji,
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Bunda Ester Bulaya , mbunge wa
Tarime, Ester Matiko na Naibu Katibu Bara, John Mnyika.
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, ilitoa dhamana kwa viongozi hao Machi 27 na
kuwapa sharti la kuripoti kituo kikuu kwenye ofisi ya RPC kila Ijumaa.
Viongozi
ambao hawajafika mpaka sasa ni Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa,
Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu na Mbunge wa Tarime,
Vijijini, John Heche.
Viongozi
hao kwa mara ya kwanza walipokea wito Februari 20, Jeshi la Polisi
likiwataka kufika kituoni hapo baada ya maandamano ya Februari 16.
0 comments:
Chapisha Maoni