Msanii
wa muziki, Diamond Platnumz Ijumaa hii amefanya mazungumzo ya siri na
Baraza la Sanaa Taifa ‘Basata’ ikiwa ni siku chache toka aingie kwenye
majibizano na Naibu Waziri wa Habari, Juliana Shonza.
Muimbaji
huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo “African Beauty” alitua viwanja
vya basata jana mchana akiwa na meneja wake, Sallam SK. Hata hivyo
baada ya kufanya mazungumzo hakuweza kuzungumza chochote juu ya nini
kilitokea.
Habari
za uhakika kutoka ndani ya Basata zinadai muimbaji huyo alifika katika
taasisi hiyo ya malezi ya wasanii kwaajili ya kuzungumza na viongozi hao
juu ya kauli zake ambazo amekuwa akizitoa juu ya Naibu waziri huyo.
Hata hivyo Basata hawajatoa taarifa yoyote juu ya kikao hicho cha siri ambacho kilichukua masaa kadhaa.
Wadau wa mambo ya sanaa wanadai huwenda muimbaji huyo alikwenda Basata kwaajili ya kuomba radhi juu ya mambo yanayoendelea.
Mapema
wiki hii muimbaji huyo wakati anahojiwa na kituo cha redio cha Times FM
aliitupia lawama Basata pamoja na Naibu waziri huyo baada ya kufungia
nyimbo 15 za wasanii wa bongofleva zikiwemo zake mbili.
Kauli
hizo zilimfanya Waziri wa Habari, Dk Mwakyembe kutoa kauli yake na
kudai kwamba ameshtushwa na kauli za muimbaji huyo juu ya waziri.
0 comments:
Chapisha Maoni