test

Jumatatu, 24 Oktoba 2016

Breaking News: Kocha wa Yanga Ajitumbua Mwenyewe


SIKU moja baada ya kocha George Lwandamina raia wa Zambia kutua nchini kwa ajili ya kusaini mkataba wa kuifundisha Yanga, kocha mkuu wa timu hiyo, Hans Pluijm ameandika barua ya kujiuzulu nafasi hiyo kuanzia leo.

Habari za kubadilishwa kwa benchi la ufundi la Yanga zilikuwepo kwa zaidi ya wiki sasa na Pluijm hakupewa taarifa yoyote hata pale alipowasili Mzambia huyo hapo jana bado uongozi wa Yanga ulisisitiza kuwa ni mwajiriwa wao halali.

Habari za uhakika ambazo BOIPLUS  imezipata ni kwamba Pluijm hajafurahishwa na maamuzi ya viongozi wa Yanga kumleta mbadala wake pasipo kumpa taarifa zozote huku yeye wakiendelea kumwambia kuwa bado ni kocha wao.

Pluijm amepanga kuwaaga wachezaji wake kesho kwenye mazoezi ya asbuhi na kueleza kuwa Yanga italazimika kumlipa kocha huyo mshahara wa mwezi mmoja huku tayari zikiwepo taarifa za kwamba Lwandamina angesaini mkataba wa miaka miwili muda wowote kuanzia leo.

Maamuzi hayo yatakuwa magumu kwa timu ya Yanga ambayo keshokutwa inakabiliwa na mechi dhidi ya Ruvu Shooting itakayochezwa Uwanja wa Uhuru ikiwa imetoka kuifunga Kagera Sugar bao 6-2 na kukusanya pointi 21 ilishika nafasi ya pili.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx