Mbunge
wa Arusha Mjini Mhe. Godbless Lema leo April 27, 2018 amekamatwa na
polisi na kufunguliwa kesi mpya kuhusu uchochezi kwa ndoto aliyowahi
kuota kuhusu Rais Dkt. John Pombe Magufuli miaka miwili iliyopita.
Mkurugenzi
wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema
amethibitisha hilo na kusema kuwa Lema leo alihudhuria Mahakamani kwa
ajili ya kesi iliyokuwa ikimkabili kuhusiana na ndoto alizoota miaka
miwili iliyopita.
"Jeshi
la Polisi Mkoani Arusha limemkamata Mbunge wa Arusha Mjini Godbless
Lema kwa kile kinachodaiwa "uchochezi". Dhidi ya Mh Rais kuhusiana na
ndoto aliyowahi kuota. Lema alihudhuria Mahakamani siku ya leo kwa ajili
ya kesi iliyokua ikimkabili kuhusiana na ndoto alizoota miaka 2
iliyopita. Baada ya Mahakama kufuta kesi hiyo leo na kuachiwa...Polisi
walimkamata tena na kumfungulia kesi upya kwa mashtaka yale yale"
alisema John Mrema
Kesi
hii ni mwendelezo wa kesi iliyokua ikimkabili Mh Godbless Lema na
ambayo ilimsotesha Mahabusu (Magereza) kwa zaidi ya miezi 4 mwaka juzi
kabla ya kuachiwa kwa dhamana mapema mwaka jana.
0 comments:
Chapisha Maoni