Rais
John Magufuli amewaonya viongozi wenye migogoro hususani wilayani
Kondoa, kuacha kutofautiana na wakae pamoja ili kuyamaliza matatizo yao
na kusisitiza pande zote zenye migogoro kuanza upya na kwamba siyo kila
tatizo lazima lifikishwe kwake.
Rais
Magufuli amefunguka hayo leo Ijumaa mjini Kondoa wakati wa ufunguzi wa
barabara ya Dodoma hadi Babati yenye urefu wa kilomita 251.
Amesema,
Tanzania ni moja na watu wote wanahitaji maendeleo hivyo migogoro ya
baadhi ya vingozi inachelewesha maendeleo ya wananchi.
"Viongozi
wa Kondoa muache kugomba leo nimeona niwape meseji live muache
kugombana niliwateua mimi nitawatoa mimi. Kuna wakati unakuta Hanang na
Kondoa wanagombania mipaka utafikiria ni nchi jirani hilo nalo linakaa
muda mrefu hata viongozi wanashindwa kulitatua hivyo ifike mahali
tumalize migogoro hii" Rais Magufuli.
Ameongeza
"Siyo kila mgogoro, lazima uletwe kwa rais. Nitaimaliza mingapi?
Viongozi waliopo washughulikie migogoro ya saizi yao. Tanzania ni kubwa
na inachangamoto nyingi, hivyo ninyi ni viongozi mnatakiwa muelewane kwa
manufaa ya wananchi wenu. Nafahamu viongozi hampendi kuzungumzwa
hadharani. Mimi nazungumzaga tu ndiyo tatizo langu. Naomba mkaniombee
labda nibadilike," amesema rais Magufuli.
0 comments:
Chapisha Maoni