Kamati
ya Bunge ya Huduma za Maendeleo ya Jamii imeuponda utaratibu unaotumika
na Serikali wa kufungia nyimbo za wasanii, zisizoendana na maadili ya
kitanzania kwa maelezo kuwa unaleta changamoto kwa wasanii.
Akiwasilisha
maoni ya kamati hiyo kuhusu bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo mwaka 2018/19 kwa niaba ya mwenyekiti wake Peter
Serukamba, mbunge wa Ludewa (CCM), Deogratius Ngalawa amesema vyombo
vinavyohusika na usimamizi vinapaswa kuhakikisha vinatimiza majukumu
yake kwa kukagua nyimbo zote za wasanii kabla hazijatoka.
“Lengo
ni kuhakikisha hakuna wimbo unaotoka kama haujazingatia maadili.
Kuangalia nyimbo ambazo ni za kimataifa na kuzipa kibali maalum kwa
maana ya muda na mahali pa kuutumia wimbo huo kabla haujaanza kutumiwa
na vyombo vya habari.
0 comments:
Chapisha Maoni