Mbunge
wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Msukuma amesema kufungia nyimbo za
wasanii nchini si jambo sahihi kwa maendeleo ya wasanii hao.
Akizungumza
katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo waka 2018/19, Msukuma amesema wasanii nchini wanalenga soko la
kimataifa, kwamba haiwezekani wapeleke video za nyimbo zao, katika soko
la kimataifa, ikiwamo Marekani wakiwa wamerekodi huku wamevaa madela.
Amesema
ni jambo lisiloingia akilini watu kutazama video za mwanamuziki Rihanna
katika vituo mbalimbali vya televisheni, huku wahusika wakiwa wamevaa
nusu utupu, huku zile za Tanzania zikifungiwa.
“Mtu
kaimba wimbo mwaka mzima uliopita leo waziri unaibuka na kufungia. Huko
vijijini watu wameshaipata hizo nyimbo, mnatupa taabu sana huko
vijijini maana watendaji wanakamata kompyuta za watu zenye nyimbo
zilizofungiwa,” amesema Msukuma.
“Msitumie
muda mwingi kufungia nyimbo, tumieni muda mwingi kuwaelimisha hawa
wasanii maana wanatumia muda mrefu sana kutengeneza nyimbo zao.”
0 comments:
Chapisha Maoni