Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB), imesema haitasoma hotuba wala taarifa
zake bungeni endapo utaratibu wa kuziwasilisha kwa Katibu wa Bunge hatua
ya kuhaririwa kwanza kabla ya kusomwa bungeni itaendelea.
Pamoja na hayo, wamesema hawatatusa bunge kwa ajili hiyo wala sababu nyingine yoyote.
Mwenyekiti
wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amesema hayo jana
Mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
mustakabali wa wabunge hao kuhudhuria vikao vya bunge na kuhusu
kukataliwa kusomwa kwa hotuba yao bungeni jana.
Mbowe
alisema anamshangaa Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson kukataa kutosomwa kwa
taarifa ya kambi hiyo bungeni jana kwa sababu tu haikuwasilishwa kwa
Spika siku moja kabla ya kusomwa bungeni.
“Naibu
Spika anasema hotuba ya KUB haipo wakati anajua kambi ilikuwa ina
watumishi wanne ambao walikuwa wanafanya utafiti, kuandaa randama ya
serikali, kuandaa hotuba zote zikiwamo za serikali sasa watumishi hao
tangu Desemba mikataba yao iliisha na niliandika dokezo kuomba wapewe
mkataba upya hadi sasa Katibu wa Bunge amekataa kufanya hivyo akidai
Spika wa Bunge yuko nje kwa matibabu.
“Sawa
walitaka hotuba hiyo niiandikie Segerea, kwa sababu wale vijana ndiyo
walikuwa wakifanya hayo na bunge lina watumishi wa mikataba 30 wakiwamo
wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, wote wana mikataba ya miaka miwili
miwili lakini wengie wako ofisini isipokuwa wa kambi ya upinzani ambao
walikufukuzwa kama mbwa katika bunge la Januari,” alisema Mbowe.
Pamoja
na mambo mengine, Mbowe amesema hapatakuwa na hotuba ya Kambi Rasmi ya
Upinzania Bungeni hadi watumishi warejeshwe lakini pia hata
watakaporejeshwa, hawatakuwa tayari kupeleka hotuba zao kwa katibu wa
Bunge akachague ni nini cha kusoma bungeni na nini cha kuacha na kwamba
Bunge liking’ang’ania kufanya hivyo, hawatasoma hotuba hizo.
Akizungumzia
suala hilo, Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai alisema bunge lina
watumishi wa kutosha kuhudumia wabunge na ofisi zao.
Alisema
hadhani kama aliyozungumza Mbowe yatakuwa na ukweli wowote kwa sababu
bunge linahudumiwa na Sekretarieti ya Bunge na watumishi wake
walioajiriwa na kuhudumia wabunge.
“Hatujakosa
sekretarieti, nina watumishi wa kutosha kuhudumia wabunge.Kulikuwa na
watumishi wa mkataba ambao mkataba wao ulimalizika Desemba, sasa
alitakiwa kusema kama anawahitaji hao lakini mwenye uwezo wa kusema
waendelee au wasiendelee ni Tume ya Utumishi wa Bunge.
“Kwangu alikuja akaniambia lakini sasa mimi ni mtumishi wa Bunge na kama unavyofahamu Spika wa Bunge alikuwa nje kwa matibabu.
“Watumishi
walioajiriwa na Bunge wapo, mimi nikiwa mmojawapo kama mbunge
anawahitaji anapewa lakini si kwa kazi binafsi. Kama anataka watumishi
wa bunge kumhudumia yeye peke yake hiyo ni juu yake, wanaweza kuwa
hawataki lakini sisi hatuwezi kuwalazimisha,” amesema Kagaigai.
0 comments:
Chapisha Maoni