test

Jumatano, 2 Novemba 2016

Serikali Yawatumbua Watumishi 1663 Kwa Kuzalisha Watumishi Hewa



Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma
Watumishi wa Umma 1,663 kutoka Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa, na Mamlaka za Serikali za Mitaa wamechukuliwa hatua za kinidhamu baada ya kubainika kusababisha watumishi hewa 19,629 hadi Oktoba 25, 2016.
 
Waziri ya Nchi, Ofisi ya Rais, anayeshughulikia Utumishi na Utawala Bora Angella Kairuki amesema hayo jana Bungeni mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mainda Hamad Abdallah (Mbunge wa Viti Maalum) alilohoji hatua zilizochukuliwa na Serikali dhidi ya watumishi waonarudisha nyuma maendeleo ya nchi.
 
Akifafanua idadi hiyo, Waziri Kairuki alisema kuwa idadi ya watumishi waliochukuliwa hatua za kinidhamu kutoka Wizara mbalimbali ni 16, Idara zinazijitegemea na Wakala za Serikali watumishi tisa, Sekretarieti za Mikoa watumishi sita na Mamlaka za Serikali za Mitaa watumishi 1,632.
 
Waziri Kairuki alisema kuwa watumishi hao wameisabishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh. bilioni 19, huku Halmashauri ya Kinondoni ikiwa na watumishi hewa 107 ambao waligharimu Serikali sh. bilioni 1.29, Kishapu watumishi 73 wamesababisha hasara ya kwa kugharimu sh. milioni 543 na kuonya kuwa waajiri waendelee kuchukua hatua za haraka na kudhibiti uwepo wa watumishi hewa ili kuipunguzia Serikali kuingia hasara kubwa badala ya kuwahudumia wananchi.  
 
Aidha, Waziri Kairuki alisema kuwa jumla ya watumishi 638 wamefunguliwa mashtaka polisi, watumishi 50 wanafanyiwa uchunguzi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na watumishi 975 mashtaka yao yamefikishwa kwenye Mamlaka zao za kinidhamu.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx