Mwenyekiti
wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB), Freeman Mbowe amesema
amenyang’anywa gari la serikali alilokuwa akitumia na Ofisi ya Bunge
ambalo ni haki yake kuwa nalo.
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini Dodoma jana Jumatano Aprili 4, Mbowe
alisema amenyang’anywa gari hilo tangu Januari, mwaka huu.
“Sina gari la serikali wala dereva, nilinyang’anywa tangu Januari natembelea gari binafsi kwa sasa, licha ya kuwa ni haki yangu.
“Lakini
mimi sijililii mwenyewe, ninayo magari mengi nitatumia na hata nikikosa
wabunge hapa watanipa gari la kutembelea,” alisema Mbowe bila kuelezea
zaidi sababu za kunyang’anywa gari hilo.
Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai akijibu tuhuma hizo amesema gari lipo isipokuwa Mbowe mwenyewe ndiyo hataki kulitumia.
“Gari la kiongozi wa upinzani lipo na dereva yupo, ila Mbowe halitaki gari wala dereva,” amesema Kagaigai.
0 comments:
Chapisha Maoni