Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amesema kuna ubadhirifu wa Sh1.5
bilioni kwenye mradi wa maji katika wilaya za Kondoa na Chemba ambao
unasuasua.
Dk
Mahenge amesema hayo leo Aprili 27 Kondoa, Dodoma wakati wa hafla ya
uzinduzi wa barabara ya Kondoa – Babati yenye urefu wa kilomita 251
inayozinduliwa na Rais John Magufuli.
Mkuu
huyo wa mkoa amesema mradi huo ulitengewa Sh2.8 bilioni kwa ajili ya
wilaya hizo lakini kulitokea ubadhirifu wa Sh1.5 bilioni. Amebainisha
kwamba vyombo vya dola vinaendelea na uchunguzi wa ubadhirifu huo.
“Tayari
vyombo vya dola vinafanya uchunguzi wa ubadhirifu wa fedha hizo.
Dhamira ya Serikali iko pale pale kuhakikisha kwamba maji yanapatikana
katika mkoa wa Dodoma,” amesema mkuu huyo wa mkoa.
Dk
Mahenge amesema Serikali imetenga Sh70 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa
miundombinu katika mkoa huo. Amesema kwenye sekta ya maji, Serikali
imeanza ujenzi wa visima vitano ambavyo vitasaidia kukidhi mahitaji ya
maji katika mkoa huo.
0 comments:
Chapisha Maoni