Mbunge
wa kuteuliwa, Abdallah Bulembo (CCM), amemtaka Waziri wa Viwanda,
Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage kuweka kando kigugumizi
alichonacho katika kuwanyang’anya wamiliki wa viwanda walioshindwa
kuviendeleza.
Bulembo
ametoa kauli hiyo jana Mei 11, bungeni jijini Dodoma wakati akichangia
makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka
2018/19, na kuongeza kuwa inashangaza kuona Mwijage anashindwa
kuwachukulia hatua wamiliki hao ilihali tayari Rais John Magufuli
alimwagiza kutekeleza agizo hilo mara kadhaa.
“Viwanda
vingi vilibinafsishwa na wamiliki wengi wameshindwa kuviendesha,
serikali na Rais magufuli amekuambia wanyang’anye… kuna watu wamepewa
vina mashine lakini hakuna kitu.
“Baadhi
ya viwanda kule Dar es Salaam, Mara , Lindi na Bukoba, wamiliki
wamevichukua na kuvigeuza kuwa maghala, sasa unaogopa nini
kuwanyang’anya ilihali tayari wamekiuka masharti ya mkataba,” alisema
Bulembo.
Bulembo
alisema watendaji walioko chini ya waziri wanamhujumu Mwijage kwa kuwa
wanaamini nafasi ya uwaziri ni ya kisiasa kwa kuwa baada ya miaka mitano
atakuja kiongozi mwingine.
“Ukipanga
nyumba ya mtu ukakuta ina nondo kesho ukiweka mbao mwenye nyumba
akikufukuza utampeleka mahakamani? wengine wana viwanda wanachechemea
afadhali hao kuliko ambao wamebadilisha matumizi,” amesema.
0 comments:
Chapisha Maoni