Mwanasheria
TSNP, Mkurugenzi wa Idara ya Sheria TSNP, Paul Kisabo amesema kuwa ni
takribani wiki sasa Mwenyekiti wao wa Mtandao wa Wanafunzi(TSNP), Abdul
Nondo amekuwa akihitajika uhamiaji ili akahojiwe uraia wake na pamoja na
wazazi wake.
Kisabo
ameeleza kuwa jambo hilo la kuhojiwa uraia wake wamelitimiza jana baada
ya kutoka Mahakama Kuu kwenye kesi yake iliyohairishwa mpaka tarehe 11,
April mwaka huu.
Aidha
ameeleza kwamba Kwa muda wa takribani wiki moja mpaka sasa mwenyekiti
wa TSNP Abdul Nondo amekuwa akihitajika uhamiaji ili akahojiwe kuhusu
taarifa za uraia wake pamoja na za ndugu zake.
Ameeleza kuwa Nondo hakupata nafasi ya kwenda sababu hakuwa sawa kutokana na changamoto alizokumbana nazo siku za hivi karibuni.
"Mnamo
sa sita mchana tuliweza kumfikisha Abdul Nondo makao makuu ya ofisi za
uhamiaji mkoa (makao makuu ya wizara ya mambo ya ndani) na wanataka
kupata taarifa zake binafsi, za wazazi wake, babu na bibi zake pande
zote mbili (upande wa baba na upande wa mama) pamoja na za ndugu
zake,kwani Afisa uhamiaji mkoa alitamka kuwa sheria inawaruhusu kumuhoji
mtu yeyote wanaotilia mashaka uraia wake.
"Wanamashaka
na uraia wa Abdul Nondo, hivyo alitakiwa awathibitishie kuwa yeye ni
raia wa Tanzania. Nondo amejaza taarifa zile anazozifahamu tu.
"Baada
ya kujaza taarifa hizo, ametakiwa kupelea cheti chake cha kuzaliwa
pamoja na vyeti vya wazazi wake wote wawili, babu na bibi zake mnamo
April 20, 2018. "Amesema Kisabo
0 comments:
Chapisha Maoni