Serikali imesema wanafunzi wa vyuo vikuu wanaongoza kutukana na kutumia lugha zisizo na maadili kwenye mitandao ya kijamii.
Angalizo
hilo limetolewa na naibu waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,
William Ole Nasha Jumamosi Machi 24, 2018 katika hafla fupi ya uzinduzi
wa Unilife Compus iliyopo Mkoa wa Kilimanjaro uliofanyika katika Chuo
Kikuu cha Mwenge na kuvikutanisha vyuo vikuu vyote vya mkoa huo.
Alisema yapo mambo matatu ambayo yanachangia wanafunzi kutofanya vizuri, yakiwamo matumizi
mabaya ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), anasa na
starehe zilizopitiliza na kujiingiza kwenye siasa ambazo zinawanyima
fursa ya kusoma vizuri.
“Serikali
imebaini mambo yanayochangia kufifisha na kudidimiza jitihada za elimu
tunayoitoa kuonekana bure. Kuna vitu ambavyo siyo vizuri vinaendelea
katika vyuo vyetu, ndizo changamoto tunatakiwa kukabiliana nazo. Chuoni
unaweza kutengeneza au kuharibu maisha yako,” alisema.
Naye
mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira alisema wanafunzi wengi
hawataki kujifunza kwa kutumia muda vizuri kwa kusoma vitabu.
"Tunabaki
kuwa waigaji wa dhana za wenzetu wa magharibi, hatutaki kujifunza vitu
vipya bali vilevile vya wenzetu vinatumika hadi leo. Wasomi wa Tanzania
tunajishusha kwa sababu ya kushindwa kuleta mawazo mapya kwenye sekta ya
elimu na afya," alisema Mghwira.
0 comments:
Chapisha Maoni