Mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe na vigogo wengine wanne wa chama hicho
walioripoti Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam leo asubuhi
Machi 27, 2018, wamewekwa mahabusu.
Viongozi
wengine waliofika kituoni hapo ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk
Vincent Mashinji; manaibu katibu wakuu, John Mnyika (Bara) na Salum
Mwalimu (Zanzibar) na Mweka Hazina wa Baraza la Wanawake Chadema
(Bawacha), Esther Matiko.
Wakili
wa viongozi hao wa Chadema, Frederick Kihwelo amesema kuwa wamefutiwa
dhamana kwa kuwa wanapotakiwa kuripoti polisi, baadhi yao hushindwa
kutokea.
Viongozi
hao waliripoti polisi Machi 22, 2018 na kutakiwa kuripoti leo. Siku
hiyo Mdee na Matiko hawakuwepo huku Mnyika na Heche wakihojiwa kwa zaidi
ya saa mbili kutokana na kutoripoti siku za nyuma.
Februari
20, 2018 Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam iliagiza kukamatwa
viongozi saba waandamizi wa Chadema, siku chache baada ya tukio la
kuuawa kwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Usafirishaji (NIT),
Akwilina Akwilini.
Akwilina
aliuawa kwa kupigwa risasi Februari 16 akiwa ndani ya daladala eneo la
Mkwajuni, Kinondoni wakati polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chadema
waliokuwa wakienda ofisi za mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni kudai
viapo vya mawakala wao.
0 comments:
Chapisha Maoni