Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad
amesema deni la Taifa linatia wasiwasi hivyo Serikali inatakiwa kuchukua
hatua kupunguza ukubwa wa deni hilo.
Profesa
Assad ametoa kauli hiyo leo Jumanne Machi 27, 2018 na kubainisha kuwa
deni hilo ni Sh46 trilioni kutoka Sh41 trilioni la mwaka uliopita,
kwamba ni ongezeko la asilimia 12.
Ametoa
kauli hiyo leo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa uwasilishaji wa
ripoti yake ya ukaguzi mwaka 2016/17 iliyobaini madudu Serikali za Mitaa
na Mashirika ya Umma.
“Tulichosema
hapa kwa kweli ukuaji wa deni tunasema ni himilivu lakini jinsi
linavyoongezeka tunakaribia maeneo ya wasiwasi. Asilimia 72 ya GDP (Pato
la Taifa) siyo mbaya lakini ikifika asilimia 76 nchi nyingine zimepata
shida, inabidi tuangalie sasa namna gani tunaweza ku-control ukuaji wa
deni hilo,” amesema.
0 comments:
Chapisha Maoni