Wakili
wa viongozi wa Chadema, Frederick Kihwelo amesema mbunge wa chama hicho
Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa naye ameungwanishwa na viongozi
waliowekwa mahabusu katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam.
Kihwelo amesema Mchungaji Msigwa aliitwa na alipofika polisi naye aliunganishwa na wenzake.
Viongozi hao wamefutiwa dhamana kwa kuwa wanapotakiwa kuripoti polisi, baadhi yao hushindwa kutokea.
Viongozi
waliowekwa mahabusu ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe; Katibu
Mkuu wa chama hicho, Dk Vincent Mashinji; manaibu katibu wakuu, John
Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar) na Mweka Hazina wa Baraza la
Wanawake Chadema (Bawacha), Esther Matiko.
0 comments:
Chapisha Maoni