Taswira
ya Vijana Tanzania (TAVITA) imelaani vikali uchochezi unaofanywa na
baadhi ya wanasiasa kupitia mitandao ya kijamii dhidi ya Serikali ya
Awamu ya tano.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam, Katibu wa TAVITA Otieno Peter alisema
Serikali ya awamu ya tano imefanya mambo mengi kama vile kuanzisha
miradi mikubwa kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania na kurejesha nidhamu
kwa watumishi wa umma.
Pia
imejikita katika kusimamia rasilimali za nchi, kuhimiza uwajibika na
kukomesha vitendo vya rushwa.Hivyo inasikitisha kuona baadhi ya watu
wakitumia muda wao mwingi kuchochea uvunjifu wa amani badala ya
kuelimisha jamii na endapo amani itapotea itakua imeharibu dira ya nchi
yetu.
Ameviomba vyombo vya habari kutumia kalamu zao katika kuelimisha kuhusu masuala ya maendeleo kwa maslahi ya Taifa.
Kwa
upande wa Mwenyekiti wa taasisi hiyo Shabani Mwanga amewataka wananchi
kutokubali taarifa zinazotolewa kwa ajili ya kuharibu taswira njema ya
nchi kwani hao wanaofanya hivyo wanataka kuvuruga amani ya nchi iliyopo.
"Kamwe
tusikubali kuyumbishwa na mawakala ambao wanatumia saa 24 kutoa taarifa
za kupaka matope ili kuharibu taswira njema ya taifa letu,"amesema .
Ameongeza
taasisi ya Taswira ya Vijana Tanzania ipo tayari kupambana kwa hali
yoyote na watu hawa wanaotaka kuchafua amani ya nchi na kwamba wapo
tayari kuunga mkono juhudi za Rais Dk. John Magufuli kwa maendeleo ya
taifa.
0 comments:
Chapisha Maoni