Mahakama
ya Mwanzo ya Wilaya ya Kinondoni, Jijini Dar es Salaam imemhukumu
msanii wa muziki wa Bongo Fleva na mjasiriamali, Zuwena Mohamed maarufu
Shilole kulipa faini ya kiasi cha shilingi milioni 14, baada ya
kupatikana na hatia ya kutapeli na kusababisha hasara kwa kushindwa
kufika kwenye tamasha.
Katika
kesi hiyo imethibitika kuwa Shilole alilipwa kiasi cha shilingi Milioni
tatu na Mary Musa ambaye ndiye muandaaji wa shoo hiyo, ili aweze
kutumbuiza siku ya mkesha wa Pasaka wa mwaka jana, 2017 katika ukumbi wa
Heineken uliopo Mbagala-Kijichi jijini Dar es Salaam, lakini hakufika
kama walivokuwa wamekubaliana.
Baada
ya mashabiki waliokuwa wameahidiwa kupata burudani kutoka kwa Shilole
kutokumuona, walipandwa na hasira na kufanya vurugu kubwa iliyosababisha
uharibifu wa mali za thamani ya shilingi milioni 14.
Kutokana
na kitendo hicho, Mahakama imemuamuru Shilole kulipa kiasi hicho cha
fedha kama fidia kwa mlalamikaji ambaye ni Mary Musa.
0 comments:
Chapisha Maoni