Naibu
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza
amemfungia msanii Roma Mkatoliki kutojihusisha na tasnia ya muziki kwa
kipindi cha miezi sita.
Akizungumza
leo Machi 1, 2018 na baadhi ya wasanii aliowaita na kuwaeleza dosari
zilizopo katika nyimbo zao, Shonza amesema baada ya Roma kupewa muda wa
kufanya marekebisho wimbo wake wa Kibamia ameshindwa kutekeleza agizo
hilo.
“Mpaka
sasa hajaufanyia marekebisho na wimbo huo unaendelea kurushwa kwenye
vyombo mbalimbali vya habari. Tulitoa muda kwa Roma kufanyia marekebisho
wimbo wake tangu mwaka jana mwishoni lakini mpaka leo ni miezi mitatu
ameshindwa kutekeleza hilo,” amesema Shonza.
Amesema jana msanii huyo alipigiwa simu ili leo afike katika kikao hicho kwa ajili ya kujitetea, pia hakutokea.
0 comments:
Chapisha Maoni