Rais
John Magufuli amewasimamisha kazi wakurugenzi wawili wa halmashauri za
Kigoma Ujiji, Boniface Nyambe na Daud Mlahagwa (Pangani).
Rais
Magufuli ametoa uamuzi huo leo Jumanne Machi 27, 2018 wakati akipokea
ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa
Mussa Assad iliyobaini madudu katika ukaguzi wa serikali za mitaa na
mashirika ya umma.
“Kuanzia
leo mkurugenzi wa Pangani na Kigoma Ujiji wasimamishwe kupisha
uchunguzi, uchunguzi ufanyike kuanzia leo lazima tuchukue hatua,”
amesema.
Akiwasilisha
ripoti hiyo, Profesa Assad amesema serikali za mitaa 140 zilishindwa
kukusanya mapato ya Sh116 bilioni ambayo ni sawa na asilimia 22 ya
mapato yake.
“Zaidi
ya hayo pia tuliona mawakala kutowasilisha Sh3.5 bilioni ya makusanyo
lakini hawakuwasilisha, ni usimamizi mbovu tu wa halmashauri kwani kama
mawakala wamekusanya kwa nini usikusanye mapato yako,” amesema Profesa
Assad.
Madudu
mengine aliyobaini CAG ni kupotea kwa vitabu 379 vya mapato ya
Serikali, ambavyo haikujulikana ni kiwango gani cha fedha kilichopotea
kutokana na upotevu wa vitabu hivyo.
“Kitabu
cha mapato kisipokuja kwetu hatuwezi kujua ni kiwango gani kimetumika
katika vitabu hivyo, lakini tuliona katika halmashauri za Bihalamuro,
Karagwe na Mpwapwa, kulikuwa na miradi mitatu ambayo thamani yake
ilifikia Sh1.6 bilioni iliyocheleweshwa kukamilishwa,” amesema.
“Pia,
kulikuwa na udhaifu katika usimamizi wa rasilimali watu na udhibiti wa
mishahara, kwa mfano kuna madai ya watumishi ambayo yanafikia Sh10
bilioni katika mamlaka za serikali za mitaa 19, ambao hawakulipa hadi
mwisho wa mwaka wa Juni 2017.”
0 comments:
Chapisha Maoni