Mkuu
wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo amefunguka na kuwaomba viongozi wa
CHADEMA jijini humo akiwepo Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema pamoja
na Meya wa Jiji la hilo, Calist Lazaro kushirikiana na serikali.
Mrisho
Gambo amesema hayo baada ya jana Machi 24, 2018 viongozi hao wa CHADEMA
ambao anadai walikuwa wamealikwa kushiriki katika zoezi la utoaji wa
mikopo kwa kina mama kutotokea kwa kuwa zoezi hilo lilikuwa likisimamiwa
na serikali.
"Nipenda
kutumia fursa hii kuwaomba viongozi wenzangu bila kujali itikadi ya
vyama vyao maana leo tulimualika hapa mbunge, Meya na madiwani lakini
wakasema tu sisi hatuendi sababu lile jambo linasimamiwa na serikali.
"Mimi nataka tu niwaombe viongozi wenzangu kwamba masuala ya maendeleo hayana vyama kwa sababu na sisi pia tungeangalia vyama pengine tungewaambia watu wa CCM wawape tu mikopo hiyo wanachama wao lakini tukasema sisi wenye serikali watu wetu ni wote bila kujali itikadi ya vyama vyao hivyo niwaombe wakubali kwamba Rais wa Tanzania ni Dkt. John Pombe Magufuli"

Aidha
Mkuu huyo wa mkoa amezungumzia suala la maandamano ya April 26, 2018
kwa namna na kusema kuwa wapo watu wanafanya kazi ya kushawishi watu
kuandamana lakini wao kama viongozi wanatoa njia za watu kupambana na
maisha.
"Wakati
wao wanahamasisha watu waandamane sisi tunawapa mbinu za kupambana na
maisha, wakati wao wanahamasisha waandamane sisi tunawagea mitaji ili
waweze kupata ridhiki na familia zao, wakati wao wanahamasisha
waandamane Dkt John Pombe Magufuli anatoa elimu bure kwa shule zote nchi
nzima" alisema Gambo.
Mwanadada
Mange Kimambi ni kati ya watu ambao wapo mstari wa mbele kushawishi
Watanzania kote nchini kupitia mitandao ya kijamii kuandamana April 26,
2018 ili kudai haki zao.
0 comments:
Chapisha Maoni