Mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe na vigogo wengine wanne wa chama hicho
wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo baada ya kuwekwa
Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam.
Viongozi
wengine waliofikishwa mahakamani hapo ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk
Vincent Mashinji; manaibu katibu wakuu, John Mnyika (Bara) na Salum
Mwalimu (Zanzibar) na Mweka Hazina wa Baraza la Wanawake Chadema
(Bawacha), Esther Matiko.
Februari
20, 2018 Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam iliagiza kukamatwa
viongozi saba waandamizi wa Chadema, siku chache baada ya tukio la
kuuawa kwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Usafirishaji (NIT),
Akwilina Akwilini.
Akwilina
aliuawa kwa kupigwa risasi Februari 16 akiwa ndani ya daladala eneo la
Mkwajuni, Kinondoni wakati polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chadema
waliokuwa wakienda ofisi za mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni kudai
viapo vya mawakala wao.
0 comments:
Chapisha Maoni