Mahakama
ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Tabora imemhukumu mkazi wa Manispaa ya
Tabora, Sadick Masunzu (47) kifungo cha miaka minne jela baada ya
kupatikana na hatia ya kumbaka binti yake mwenye umri wa miaka 16 na
kumpatia ujauzito.
Akitoa
hukumu hiyo jana, hakimu wa mahakama hiyo, Joctan Rushela alisema
ameridhika na maelezo yaliyotolewa na upande wa mashtaka uliokuwa
ukiongozwa na wakili Tito Mwakalinga kuthibitisha bila shaka kuwa
mshtakiwa alitenda kosa hilo.
Hakimu
huyo aliongeza kuwa kitendo kilichofanywa na mshtakiwa si cha kiungwana
katika jamii ya Watanzania, hivyo mahakama inamtia hatiani kwa kosa
hilo na inamhukumu kwenda jela miaka minne ili liwe funzo kwake na kwa
wengine wenye tabia kama hiyo.
Awali
wakili wa Serikali, Mwakalinga alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa
alimbaka mtoto wake wa kumzaa na kumsababishia ujauzito.
Mwakalinga
alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo katika tarehe tofauti Januari 2017
na kumsababishia ujauzito binti huyo aliyekuwa mwanafunzi wa Sekondari
ya Lwanzali iliyopo katika Manispaa ya Tabora ashindwe kuendelea na
masomo.
Upande
wa mashtaka uliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa kwa
kuwa kitendo cha kumbaka na kumtia mimba mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi
kimemharibia maisha yake.
0 comments:
Chapisha Maoni