Mkurugenzi
wa Habari na Mawasiliano wa Timu ya Simba, Haji Manara ambaye ni
mwanachama wa CCM amefunguka na kusema hajawahi kumshabiki Tundu Lissu
wala CHADEMA lakini anaamini bila uwepo wake na CHADEMA basi chama chake
CCM kitalala.
Haji
Manara amesema hayo leo baada ya kuona picha ya kwanza ya Mbunge wa
Singida Mashariki Tundu Lissu akiwa hospitali jijini Nairobi nchini
Kenya ambapo anapatiwa matibabu kufuatia kupigwa risasi Septemba 7, 2017
na watu wasiojulikana.
"Ohhh
God,mimi sijawahi kukushabikia wewe wala chama chako ila nakuombea kwa
Mungu upone haraka kaka, urudi katika harakati zako nikiamini bila uwepo
wenu chama changu kitalala" aliandika Haji Manara kupitia ukurasa wake wa Instgram.
Mbali
na Haji Manara watu wengine wengi wameonyesha kufurahishwa na hali ya
Tundu Lissu baada ya kumuona kupitia picha ambazo zimeanza kusambaa
kwenye mitandao ya kijamii, Mbunge huyo wa Singida Mashariki anatarajiwa
kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu ya awamu ya tatu siku za karibuni.
0 comments:
Chapisha Maoni