Familia
ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu imesema kwamba kwa mara ya
kwanza ndugu yao alipotolewa nje kupata hewa na kuota jua kauli yake
aliyoitoa alisema kuwa ni sawa na ukiwa mfungwa huoni jua, mawingu wala
hupigwi upepo wa kawaida.
Katika
mahojiano aliyofanyiwa Kaka wa Lissu, Wakili Alute Mughwai Lissu
amesema kwamba mara baada ya ndugu yake kutolewa nje na kukaa kwa
takribani dakika 30 siyo yeye Lissu peke yake aliyefurahi bali ndugu
wote waliokuwepo hospitalini hapo walifurahia mno hilo tukio.
Bw.
Alute amesema kwamba awali Manesi walipanga kumtoa nje Jumamosi (Oktoba
14) na kwa kuwa Lissu alijua tunakwenda, aliwaeleza wasimtoe bali
wasubiri ndugu zake wafike.
"Nilikuwa
mimi na ndugu wengine. Ilipofika saa 10 jioni tulimtoa na mimi ndiye
nilimtoa ICU, alifurahi na sisi tulifurahi kwa hatua hiyo,” amesema Kaka
huyo mkubwa wa Lissu.
Alute
ameeleza kwamba baada ya Lissu kupata upepo wa nje kwa nusu saa nzima
alirudishwa wodini ambako amefafanua siyo ICU tena ingawa pia kuna
ulinzi na uangalizi wa karibu na si kila mtu anaweza kumwona na kuongeza
kwamba hali ya ndugu yake inazidi kuimarika huku akili zake zikiwa
timamu.
Pamoja
na hayo Alute amesema kwamba suala la kumpeleka sehemu tofauti ya
matibabu ndugu yao familia ndiyo itakayoshughulika zaidi kwa ukaribu na
kuongeza kwamba, ndugu wengine wapo sehemu mbalimbali kama Kenya,
Australia, Marekani, Canada ambao watabidi wajadiliane kwanza ndipo
watatoa taarifa juu ya nini kinaendelea.
0 comments:
Chapisha Maoni