Mbunge wa jimbo la Sengerema, William Ngeleja, amesema kutuhumiwa siyo kukutwa na hatia na maisha yanaendelea.
Ngeleja
ambaye ni mmoja wa watuhumiwa waliotajwa kwenye Ripoti ya pili Rais ya
kuchunguza Makinikia, ameyasema hayo leo alipokuwa akichangia Bajeti Kuu
ya Serikali ya 2017/18.
Wakati
akiendelea na mchango wake, aliwataka wabunge kusimama ili kuonyesha
kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa kupambana na wizi wa rasilimali za
Watanzania ikiwamo dhahabu.
Wakati
akiendelea na mchango wake huo, Mbunge wa Mbozi, Pascal Haonga, aliomba
kutoa taarifa kwa mzungumzaji akimtaka Ngeleja kueleza uhusika wake
kwenye kashfa hiyo kwa sababu kamati imemtaja.
Baada
ya kauli hiyo, Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu, alimtaka Ngeleja
kuendelea na mchango wake na kuwa alichotoa Mbunge Haonga siyo taarifa.
Hata hivyo kabla ya kuendelea na mchango wake, Ngeleja alisema ” kutuhumiwa siyo kukutwa na hatia na maisha yanaendelea”.
0 comments:
Chapisha Maoni