Baada
ya Rais, Dk. John Magufuli kukabidhiwa ripoti ya mchanga wa dhahabu,
Chama cha NCCR-Mageuzi kimekitaka Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwaomba
radhi Watanzania.
Katibu
Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Juju Danda, alisema katika taarifa yake kwa
vyombo vya habari jana, kwamba ripoti hiyo ya mchanga imeanika uozo
uliosababishwa na CCM kwa kipindi kirefu ilichokaa madarakani.
“Kwa
maana hiyo, ni vema CCM wakakaa, wajiulize na kujipima kwa kuwaomba
radhi Watanzania ambao wamekuwa wakiishi maisha magumu yaliyosababishwa
na CCM.
“Kamati
mbili zilizoundwa na Rais Dk. John Magufuli, zimethibitisha pasipo
shaka, kuwa Watanzania wameibiwa tena kwa kiwango kikubwa ingawa mwaka
2007, Kamati ya Bomani ilitoa maoni na mapendekezo kadhaa yaliyohusu
sekta ya madini ingawa maoni hayo hayakufanyiwa kazi,”alisema.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo, kukiri kosa ni uungwana na kwamba CCM
wanatakiwa kujitokeza hadharani na kuwaomba radhi Watanzania, kuwa
hawakuwatendea haki kutokana wizi uliokuwa ukifanyika katika sekta ya
madini.
Pamoja
na hayo, Danda aliiomba Serikali kuhakikisha inachukua hatua za
kisheria kwa yeyote aliyeshiriki katika kuangamiza uchumi wa Taifa kwa
kusaini mikataba mibovu katika sekta ya madini.
“NCCR-Mageuzi,
tunafarijika kuona tuliyokuwa tukiyapigania kwa miaka mingi,
yanaendelea kufichuliwa waziwazi na ukweli unazidi kubainika kupitia
kamati zilizoundwa na Rais.
“Pia
ni muda muafaka wa kupitia upya sheria zote zinazohusu masuala ya
madini na ni wakati muafaka wa wataalamu wazalendo kuipitia tena Katiba
iliyopendekezwa kwa kuwa inatoa mwelekeo wa kuwadhibiti wabadhirifu,” alisema.
0 comments:
Chapisha Maoni