Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa amepiga marufuku usafirishaji wa chakula nje ya
nchi bila kibali na kuwataka wafanyabiashara kuuza chakula kwenye maeneo
yenye uhaba nchini.
Majaliwa
ametoa agizo hilo leo, Jumatatu wakati akihutubia Baraza la Eid katika
Msikiti wa Masjid Riadha mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Waziri
Mkuu huyo amesema kuwa kuna maeneo ambayo wananchi hawakupata chakula
vizuri kutokana na uhaba wa mvua hivyo wafanyabiashara wapeleke chakula
kwenye maeneo hayo.
“Serikali
bado haijatoa kibali cha kutoa chakula nje ya nchi, kama unaona kuna
umuhimu kaombe kibali, lakini utapewa kibali cha kusaga upeleke unga na
siyo mahindi,”amesisitiza Majaliwa.
Majaliwa
ameonya kuwa kwa wale watakao kamatwa wakisafirisha mahindi nje ya nchi
kinyume na utaratibu, mahindi hayo yatataifishwa na kupelekwa kwenye
ghala la Taifa na magari yatapelekwa polisi.
Amesema kuwa Serikali imepokea barua za maombi ya kupeleka chakula nchi jirani, lakini bado haijatoa ruhusa.
0 comments:
Chapisha Maoni