Mchungaji
wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo alimaarufu kama 'Mzee wa
Upako' amefunguka na kusema mtu kufa maskini si jambo la kusifiwa hata
kidogo kuwa ni uzalendo bali ni Ufala.
Mchungaji Lusekelo amesema hayo alipokuwa akiongea na mtangazaji wa kipindi cha UJENZI cha EATV kinachoruka kila Jumapili.
Mzee
wa Upako anasema mtu anapokufa akiwa ameacha mali za kutosha ni jambo
jema kwani familia yake nyuma haiwezi kupata taabu wala watoto hawawezi
kupata shida tofauti na yule anayekufa akiwa na kitanda tu kwani watoto
wake watapata shida na mateso.
"Watu
wanamsifu mtu amekufa bila mali eti alikuwa mwadilifu yaani unakuta mtu
amefanya kazi serikalini miaka na miaka, sijui miaka 35 au 40 anakufa
hata kitanda hana.
"Wapo
watu wanasema huyu jamaa alikuwa mzalendo na muadilifu sana hata
kitanda hana, hamna mtu huyo alikuwa fala umenielewa?, huyu alikuwa fala
na hastaili kuwa kielelezo cha msingi tuhoji mtu kapata mali wapi?
"Ndio
jambo la msingi sababu unaacha watoto duniani unadhani wataishi vipi?
Mama anakuwa na nyumba pale anachota kodi anapeleka watoto shule maisha
yanaendelea" alisisitiza Mzee wa Upako.
0 comments:
Chapisha Maoni