MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
Hisia za mapenzi zikazidi kupanda kati yao, mikono ya Eddy ikawa na
kazi ya kupita kila kona ya mwili wa Phidaya. Kwa nguvu alizo nazo
akamnyanyua na kumkalisha kwenye sehemu maalumu ya kunawia mikono.
Hapakuwa na mtu aliye kuwa na kipingamizi cha kumpatia mwenzake denda la
kutosha.
Kwa
haraka Phidaya akaanza kuufungua mkanda wa suruali ya Eddy, hakuishia
hapo akafungua na zipu ya suruali hiyo na kiganja chake akakiingiza
sehemu lilipo tango lililo simama kidedea.
Viganga vya Eddy vikawa na kazi ya kuyaminya minya mziwa ya Phidaya yaliyo simama vizuri.
“Eddy tizama nyuma yakoooo”
Phidaya alizungumza kwa sauti ya juu huku macho yakimtoka huku kiganja chake akikitoa sehemu lilipo tango la Eddy
ENDELEA
Kitendo
cha Eddy kugeuka nyuma, akakutana na ngumi nzito iliyo tua usoni mwake
na kumfanya apate kizunguzungu cha gafla. Kwa haraka Phidaya akaiweka
nguo yake vizuri, huku macho yake yopte yakiwa kwa mwanaume aliye jazia
misuli.
Mwanaume
huyo aliye ingia ndani ya choo hicho, kwa lengo la kujisaidia haja
ndogo. Ila alipo iona sura ya Eddy, akatambua ya kwamba ndio mtu wanaye
mtafuta katika kundi lao lenye watu wengi karibia dunia nzima. Eddy
akajaribu kusimama, ila mwanaume huyo aliye na umbo refu kwenda juu na
mwenye kifua kilicho gawanyika kwa mazoezi makali aliyo yafanya.
Akampiga Eddy teke moja lililo tua kwenye mbavu na kumfanya Eddy kutoa
ukelele mkali wa maumivu.
Phidaya
bila ya kujifikiria mara mbili akamrukia mwanaume huyo mgongoni na
kunaza kumpiga makofi ambayo kwa ukakamavu wa mwanaume huyo hayakuwa na
maumivu ya aina yoyote. Kwa nguvu alizo nazo mwanaume huyo akamshika
Phidaya kwa mikono yake yote miwili na kumrushia kwenye moja ya kioo cha
ukutani mwa choo hicho, kitendo kilicho mfanya Phidaya kugugumia kwa
maumivu makali huku damu zakimtoka kwenye upande wake wa kushoto ambao
alipigizwa kwenye kioo hicho kilicho pasuka.
Mwanaume huyo hakutaka kudili sana na Phidaya, akamsogelea Eddy ambaye
anajizoa zoa kunyanyuka kutoka chini. Akamshika kwa mikono yake yote
miwili na kumyanyua usawa wake. Akampiga Eddy kichwa kimoja cha uso
kilicho mzidisha Eddy kulegea kwa kukosa nguvu.
Akiwa
emeendelea kumshikilia Eddy akamtandika kichwa cha pili cha uso kilicho
mfanya Eddy kutulia tuli na kupoteza fahamu. Mwanaume huyo pasipo
kuchelewa, akamuweka Eddy begani mwake, akamtazama Phidaya anaye gugumia
kwa muamivu makali chini alipo lala. Akataka kutoa bastola na kumpiga
Phidaya, ila akamuonea huruma kwa maana si muhusika katika sekeseke
hilo.
Akafungua
mlango wa kutokea kwenye choo hicho. Akachungulia pande zote mbili za
kordo hiyo ndefu ila hakuona mtu yoyote akikatiza. Alipo hakikisha
usalama upo, taratibu akaanza kutoka na kutembea kwenye kordo hiyo
kuelekea nje, huku Eddy akiwa amembeba begani.
Mwaname huyo mwenye asili ya kiarabu, aliye changanyia na asili ya
Kirusi(Russia). Akazidi kutembea kwa kwa kujiamini kwenye kordo hiyo
hadi akafanikiwa kufika sehemu ya mapokezi ambapo ndipo kuna lango la
kutokea kwenye hospitali hiyo. Manesi na watu walipo kwenye eneo hilo,
wakabaki wakimshanga mwanaume huyo.
“Samahani muheshimiwa, mtu huyo unampeleka wapi?”
Askari mmoja wa ulinzi wa eneo hilo alimsimamisha mwanaume huyo, aliye mbeba Eddy.
“Ni ndugu yangu nimekuja kumchukua nimrudishe nyumbani”
“Mbona huyo ni mwafrika na wewe si muafrika imekuwaje akawa ni ndugu yako?”
Mwanaume
huyo akaka kimya huku akiwatazama askari wawili wanao sogelea eneo
hilo, baada ya kumuona mwenzao akimuhoji mwanaume huyo mwaswali.
Mwanaume huyo akamtazama askari huyo anaye muhoji maswali anayo hisi
yanampotezea wakati. Taratibu akaurudisha mkono wake wa kulia nyuma, ili
kuichomoa bastola yake aliyo ifunika na jaketi lake zito.
“Ahaaaaaaaaaa bastolaaaaaaa”
Binti
mmoja aliye kaa kiti cha nyuma ya jamaa huyo aliweza kuona kitendo
anacho taka kukifanya jamaa huyo. Askari wawili ambao wanao mfwata jamaa
huyo wakaongeza mwendo huku kila mmoja akijaribiu kuwahi kuichomoa
bastola yake kiunoni mwake. Kufumba na kufumbua wakastukia wakitupiwa
Eddy, ikawabidi wamdake na wote wakaanguka chini. Askari aliye simama
karibu yake aliye kuwa akimuhoji maswali, alistukia akitandikwa teke la
sehemu za siri lililo mfanya ajikunje huku akilia kwa maumivu makali
sana.
Askari
wengine walipo eneo hilo wakaongezeka kukabiliana na mwanaume huyo,
ambaye tayari alisha ichomoa bastola yake na kuanza kukabiliana na
askari wanamfwata huku wakiwa wameshikilia mitutu ya bunduki. Watu wote
waliopo katika eneo hilo la mapokezi walijikuta wakilala chini huku
wachache wakiamua kukimbilia nje kuyaokoa maisha yao.
Mashambulizi
ya polisi na mwauamue huyo yalizidi kuwa makali, baada ya mwanaume huyo
kujibanza kwenye moja ya nguzo iliyopo katika eneo hilo. Iliyo msaidia
kukinga risasi zinazo toka kwa askari. Macho ya mwanaume huyo muda
mwingi yaliweza kumtazama Eddy aliye lala mita chacha kutoka sehemu
alipo jificha na ni ngumu kwa yeye kuweza kumchukua kwa maana akifanya
hivyo basi risasi za askari wanao ongeze kila muda basi zinaweza kuishia
kwenye mwili wake.
Mwaname
huyo aliye fika hospitalini hapo kwa lengo la kumtembelea bibi yeka,
aliye lazwa kwenye hospitali hiyo, lengo lake liliweza kuvunjika baada
ya kuibanwa na haja ndogo na kuingia kwenye moja ya choo ambacho pasipo
kutazama kama kimewekewa tangazo la matengenezo, alijikuta akiingia tu
kuitua haja yake hiyo na ndipo hapo alipo weza kumuona Eddy akiwa na
Phidaya kwenye choo hicho wakiendelea kuogelea kwenye dibwi zito la
mahaba. Alipo hakikisha kwamba mtu huyo ndio wanaye mtafuta baada ya
kuiangalia picha ya Eddy kwenye simu yake, ndipo alipo amua kufanya
shambulizi lililo mzidi Eddy na kumchukua kiurahisi.
“F……k”
Mwanaume
huyo alizungumza huku akimtazama Eddy kwa macho ya hasira. Akachomoa
magazine ya bastola yake na kukuta ikiwa imesalia na risasi tano tu na
wingi wa askari hao ni mkubwa kuliko wingi wa risasi zake.
“I wiil be back”(Nitarudi tena)
Mwanaume
huyo alizungumza huku akijiandaa kukimbia kwa kutokea kwenye moja
mlango mmoja wa kioo uliopo mbele yake. Akaikoki bastola yake vizuri
akafyatua risaasi mbili kuelekea walipo askari, kisha akachomoka kwa
kasi kubwa, na kuwaacha askari wakifyatua risasi ambazo zote zilipita
pembeni. Mwaume huyo akadandia pikipiki yake kubwa aliyo kuja nayo na
kuondoka eneo hilo la hospitaloi kwa mwnedo kasi.
***
Milio ya risasi iliweza kusikika eneo zima la hospitalini. Mlinzi mmoja
anaye linda jengo la kuhifadhia maiti(Mochwari). Kwa woga akajikuta
akifungua mlango na kuingia ndani ya jengo hilo huku akihema. Kitendo
cha mlinzi huyo kuingia ndani ya jengo hilo Shamsa aliweza kuona sehemu
mwanga wa mlango ulipo tokea na mtu huyo kuingia ambaye hakujua kwamba
ni nani. Kwa haraka Shamsa akaanza kutembea kwa haraka kuelekea eneo la
mlango huku akiomba msaada.
Mlinzi
huyo akasikilizia sauti ya msichana huyo inayo omba msaada akahisi
labda ni wenge la woga wake, kwa maana tangu afanye kazi hiyo ni mwaka
wa kumi na mbili hajawahi kusikia wala kuona kitendo kama hicho
kilichopo mbele yake. Kwa haraka mlinzi akakimbilia swichi ya kuwashia
taa. Kwa haraka akawasha taa, eneo zima la ndani likatawala mwanga.
Macho
ya mlinzi yakakutana na macho ya Shamsa, ambaye alishuhudia akiingizwa
humu ndani maasaa machache yaliyo pita, ikisadikia kwamba amefariki
dunia.
“Usinisogelee”
Mlinzi huyo alumuambia Shamsa huku akiwa ameishia bastola yake mkononi na mwili mzima akitetemeka kwa woga.
“Naomba unisaidie kaka yangu”
Shamsa alizungumza huku akiwa amesimama, akifwata amri ya mlinzi huyo anaye onekana kuwa na woga mwingi.
“Wewe umekufa”
“Nimekufa!?”
“Ndio umekufaaa”
Mlinzi
huyo alizungumza hivyo huku akijikaza tu, ila miguu yake na mikono yake
ilionyesha kwamba anashindwa kusimama kutokana na woga mwingi ulio
mjaa. Shamsa akatazama eneo alilopo, hapo ndipo akaelewa kwamba sehemu
aliyopo ni katika chumba cha kuhifadhia maiti.
“Ahaa……ka…aaka mi sijafaaa”
Shamsa alizungumza huku machozi yakimlenga lenga.
“Tazama viungo vyangu sijafa kabisa, ona niniatembea”
Shamsa
akapiga hatua mbili mbele na kiumfanya mlinzi kuishikilia vizuri
bastola yake na kumuamrisha tena asimama alipo kwa maana haamini kama
Shamsa ni binadamu wa kawaida.
“Ukisogea nakumwaga ubongo zombie mkubwa weee”
Mlinzi huyo alizungumza huku akirudi rudi nyuma kuufwata mlango wa kutokea sehemu ulipo.
***
Sa Yoo na Raisi Praygod walibiki wakisikilizia milio hiyo ya risasi
wakiwa nje ya chumba alicho ingizwa Rahab kwa ajili ya kufanyiwa
matibabu.
“Kumevamiwa”
Raisi
Praygod alizungumza huku akihema kwa woga, wakawaona askari kadhaa
wakikatiza mbele yao wakikimbilia sehemu kunapotekea milio ya risasi. Sa
Yoo baada ya kuona hivyo na yeye akaanza kufwata kwa nyuma.
“Wee Sa Yoo rudi hapa”
Raisi
Praygod alijaribu kuita ila Sa Yoo tayari alisha fika mbali. Sa Yoo
akafika sehemu ya mapokezi. Katika kuangaza angaza Sa Yoo akamuona Eddy
akiwa amelala chini akiwa hajitambui. Mapigo ya moyo yakaanza kumenda
mbio. Kwani hakujua ni kitu gani kimempata Eddy, kila alivyo tizama
jinsi askari wakirushiana risasi na mtu aliye jificha nyuma ya nguzo
moja kubwa, huku Eddy akiwa amelala pembeni, alihisi kuchanganyikiwa.
Akataka
kwenda ila risasi moja ikatua karibu na askari aliye kaa naye pembeni
na kumfanya askari huyo kudoka chini na kanza kuvujwa damu. Sa Yoo kuona
hivyo na yeye akalala chini huku akizidi kuchanganyikiwa. Kitu kilicho
zidi kumuumiza kichwa zaidi ni jinsi Eddy alivyo baki katika sura yake
ya kawaida na hakuina sura ya bandia ambayo alitengenezewa akiwa Japani.
Sa Yoo akafanikiwa kuweza kumuona mwanaume aliye kuwa akifyatua risasi
nyingi, akichomoka kwa kasi na kutoka nje katika eneo hilo. Kwa haraka
Sa Yoo akanyanyuka kutoka katika eneo aliko kuwa amelala na kuanza
kukimbia kueleka sehemu alipo lala Eddy. Kwa haraka akapiga magoti
chini, kuitazama hali ya Eddy. Sa Yoo akaanza kuuchunguza mwili wa Eddy
kama umejeruhiwa na risasi, ila hakukuta damu yoyote, ila usoni mwa Eddy
kidogo kukawa na mabadiliko. Pua ya Eddy kidogo iliuweza kuvimba
hakujua ni nini kilicho ifanya pua hiyo kuvimba.
“Msaadaa jamani”
Sa
Yoo alizungumza kwa sauti ya juu. Menesi na madaktari wakaanza
kuwashuhulikia askari majeruhi walio jeruhiwa kwa risasi ikiwemo na
Eddy. Sa Yoo hakutaka kukaa mbali na Eddy akanza kufwata nyuma kitanda
cha matairi alicho lazwa Eddy kinacho sukumwa na manesi wawili.
Eddy
akaingizwa kwenye chumba cha huduma ya kwanza, akawekewe mirija ya gesi
puani mwake. Sa Yoo hakuruhusiwa kuingia kwenye chumba hicho.
“Madam Phidaya”
Sa
Yoo alikumbuka huku akiangaza macho yake huku na kule, hakujua ni wapi
alipo. Kumbu kumbu ya mwisho aliyo ikumbuka ni jinsi Eddy alivyo ondoka
na Phidaya huku akimburuta kutoka katika eneo la ugomvi. Kwa haraka Sa
Yoo akaanza kutembea kuelekea katika sehemu ambayo walimiucha madam
Mery. Hakutumia dakika nyingi akawa amesha fika katika eneo hilo ambapo
akamkuta Madam Mery akiwa amejiinamia kwenye kitia alicho kaa.
“Madam Mery umemuona wapi Madam Phidaya?”
Sa
Yoo aliuliza swali ambalo fika alitambua kwamba hato jibiwa sahihi.
Madam Mery akanyanyua sura yake na kumtazama Sa Yoo kisha akajibu kwa
kutingisha kichwa kwamba hatambui ni wapi alipo.
“Mungu wangu, sasa itakuwaje?”
Sa
Yoo alizungumza huku jasho likimwagika. Madam Mery akamtazama Sa Yoo
usoni mwake na kutambua kuna kitu ambacho kinaendelea kwa maana sura
yake imejawa na masha makubwa sana.
“Kuna nini kimetokea?”
“Eddy amevamiwa na majambazi”
“Ehheee……..!!?”
Madma Mery alishaanga huku akisimama kwenye kiti, habari hiyo fika ilionyesha kumstua sana Madam Mery.
“Yuu…….uuuu..po wapi Edddy”
“Yupo wodini anashuhulikiwa, hapa ninamtafuta madam Phidaya”
Kutokana
na mawazo mengi Madam Mery aliisikia miliio ya risasi ila
hakujishuhulisha nayo, alihisi labda ni mawazo yake ndio yanayo mtuma
hivyo. Sa Yoo akaitazama korodo ambayo Eddy na Phiday waliondoka
pamoja.
Bila
hata ya kuuliza akaanza kutembea kwa mwendo wa haraka kuifwata kordo
hiyo iliyo ndefu na iliyo tulia, huku madam Mery naye akifwata kwa
nyuma. Wakapita kwenye mlango wa choo, kilicho wekwa tangazo kwamba kipo
katika matengenezo. Sa Yoo hakukitilia maanani sana, hatua mbili mbel,
akasikia sauti ya mtu akigugumia kwa maumivu kutoka katika choo hicho.
“Vipi?”
Madam
Mery aliuliza baada ya kumuona Sa Yoo akisimama na kugeuka nyuma. Sa
Yoo hakujibu chochote zaidi ya kuanza kurudi taratibu huku masikio yake
yote na macho akiwa amevielekezea inapo tokea sauto hiyo. Akautazama
vizuri mlango wa kuingilia chumba hicho, akakuta ukiwa wazi kidogo,
taratibu akausukuma na kuingia ndani. Hakuamini macho yake baada ya
kumkuta Phidaya akiwa amekaa kitako akijitahidi kunyanyuka. Vipande vya
vioo vilivyo anguka chini vilizidi kumkata kata Phidaya pale alipo
jaribu kuweka mikono yake chini ili anyanyuke.
“Madam”
Sa Yoo alizungumza huku kwa haraka huku akimfwata Phidaya. Kwa kusaidiana na Madam Mery wakamnyanyua.
“Eddy ametekwa jamani”
Phidaya alizungumza kwa shinda huku akimtazama Sa Yoo usoni.
“Yupo yupo tayari amesha okolewa na polisi”
Sa
Yoo alijibu kwa haraka. Madam Meri aliweza kuiona sura ya bandia ya
Eddy aliyopo juu ya sinki la kunawia mikono. Akaiokota kisha wakatoka
katika choo hicho. Madam Mery hakujali tofauti zilizopo kati yake na
Phidaya. Moja kwa moja wakaeleka katika chumba ambacho Eddy anapatiwa
huduma ya kwanza. Manesi wakampokea na Phidaya, wakaanza kumshuhulikia.
***
“Samahani kaka usitoke, mimi sio Zombi”
Shamsa
alizungumza huku akizidi kumfwata mlinzi aliye simama karibu na
mlangoni. Mlinzi akazidi kutetemeka hadi bastola ikamdondoka chini.
Ikawa ni nafasi nzuri kwa Shamsa kutembea kwa mwendo wa haraka hadi
karibu kabisa na mlinzi huyo, kitendo cha kumshika mlinzi huyo aliye toa
macho kwa woga. Mlinzi akaanguka chini na kupoteza fahamu.
Shamsa
akashangaa sana, hakutaka kupoteza muda akamfungua mlango na kutoka
eneo hilo. Milio ya risasi ikamfanya agundue kuna tatizo katika eneo
hilo la hospitalini kwa haraka akaanza kutembea kueleka inapo tokea
milio hiyo ya risasi ili kuweza kujua ni nini kitanacho endelea.
Akafika
karibu na lango la kuingilia katika eneo la mapokezi, ila mwanaume
mmoja mrefu akachomoka kwa kasi na kudandika pikipiki na kuondoka kwa
kasi. Akabaki kumshangaa mwanaume huyo anavyo tokomea kwenye geti la
kutokea katika eneo la hospitali.
Mwanaume
huyo anaye onekana kuto kuwa na huruma, alimbabiza teke moja mtoto
mmoja mlemavu wa miguu anaye tumia kiti cha magurudumu kutembelea,
akaangukia pembeni na mwanaume huyo akapita kwa kasi. Kitendo hicho
kikamkera sana Shamsa na kuanza kukimbilia sehemu alipo angukia mototo
huyo.
“Umeumia?”
Shamsa
alimuuliza mtoto huyo hakujibu kitu chochote zaidi ya kugugumia kwa
maumivu makali aliyo yapata. Kwa haraka Shamsa akamnyanyua mtoto huyo
na kumuweka kwenye kiti chake. Akatoka nje ya geti hilo huku akiwa
anakimbia akamuona mwanaume aliye fanya tukio hilo akikatiza kwenye moja
ya barabara. Katika kuangaza angaza macho upande wa pili akaona
sharobaro mmoja akishuka kwenye moja ya pikipiki kubwa na nzuri ya
kifahari na kuingia dukani.
Kwa
kasi Shamsa akakatiza kwenye barabara hiyo, akaifikia pikipiki hiyo kwa
bahati nzuri akakakuta funguo ikiwa juu ya pikipiki hiyo. Kwa haraka
akaidanda pikipiki hiyo na kuondoka eneo hilo kwa kasi na kumfanya
sharobaro huyo kutoka nje ya duka hilo kushuhudia pikipiki yake
inavyotokomea, kitendo kilicho mfanya amwagikwe na machozi.
Kwa
bahati nzuri Shamsa akafanikiwa kumuona mwanaume huyo kwa mbali
akizidi kutokomea katikati ya barabara yenye magari mengi yanayo kwenda
kwa kasi. Kitu kilicho mfanya Shamsa kuzidi kuongeza mwendo kasi wa
pikipiki yake na kuzidi kumsogelea mwanaume huyo ambaye bado hajafahamu
ni nini alicho kitenda ndani ila kwa kitendo alicho mfanyia mtoto
mlemavu akaapa ni lazima amtie mikononi mwake na alipe kwa kitendo
hicho.
SORRY MADAM (75) (Destination of my enemies)
Shamsa
akajaribu kadri ya uwezo wake kumfukuzia mwanaume huyo ila, akashindwa
kutokana na msongamano wa magari kuwa mengi na kitu kingine kilicho
mfanya kumpoteza mwanaume huyo ni pale magari ya upande wake yalipo
simamishwa na taa za barabarani zinazo ongoza magari hayo.
“Shitiitiiii”
Shamsa
alizungumza huku akigeuza na kupita barabara nyingine kurudi
hospitalini. Safari haikumchukua muda mwingi akwa amefika hospitalini.
Lengo la yeye kufika hapo ni kutaka kujua ni kitu gani kilicho sababisha
hadi akapelekwa katika jengo la kuhifadhia maiti. Hali ya ukimya na
ulinzi mkali aliyo ikuta mapokezi, haikumshangaza sana kwa maana naye
aliweza kuisikia miliyo ya risasi.
“Samahani nesi?”
Alimuuliza nesi mmoja aliye kaa kwenye moja ya dirisha la mapokezi.
“Bila sahamani?”
“Kuna jambo ambalo linanichanganya kidogo?”
“Jambo gani?”
Shamsa
akaka kimya huku akipangilia ni kitu gani atamuelezea nesi huyo hali
ambayo imetokea. Ila kabla hajazungumza kitu cha aina yoyote akastukia
akishikwa bega kwa nyuma.
***
Eddy akazinduka kutoka katika usingizi mzito alio kumbana nao kwa
kipigo alicho pigwa na mwanaume ambaye hakumtambua. Macho yake
yakaangaza chumba kizima. Akamuona Sa Yoo akiwa amesimma pembeni yake
huku Phidaya akiwa amekaa kwneye moja ya kiti akiwa amefungwa bandeji.
Akageuka upande wa pili akamuona Madam Mery akiwa ameegemea ukuta.
“Vipi?”
Eddy alimuuliza Sa Yoo aliye tazamana naye.
“Safi unajisikiaje?”
“Ahaaa kichwa kinaniuma”
Taratibu Phidaya akanyanyuka kutoka katika kiti alicho kaa na kupiga hatua hadi kitandani na kukaa pembeni mwa kitanda.
“Honey pole”
“Asante mke wangu, vipi umeumia sana?”
“Hapana ni chupa chupa ndio zimenichoma kwenye mkono”
“Pole”
Taratibu Phidaya akainama na kumbusu Eddy mdomoni kwa mahaba makubwa sana.
“Muheshimiwa raisi yupo wapi?”
“Ahaa ngoja nikamtazame kwenye wodi alipo lazwa Rahab?”
Sa
Yoo baada ya kuzungumza hayo akatoka ndani ya chumba hicho na moja kwa
moja akaelekea hadi kwenye wodi aliyo lazwa Rahab, akamkuta Raisi
Praygod akimsaidia Rahab kukaa kitako kwenye kitanda.
“Madam Rahab umeamka?”
“Ndio, vipi Eddy yupo wapi?”
Swali
la Rahab kumuulizia Eddy likamfanya raisi Praygod kuguna kimoyo moyo,
kwa maana alihisi labda mke wake atafurahia uwepo wake hapo.
“Eddy naye yupo kwenye wodi amelazwa?”
“Amelazwa?”
“Ndio, alivamiwa na jambazi ambaye hajulikani?”
“Mmmm, ilikuwaje akavamiwa?”
“Hata mimi sifahamu, ila amesha ivua sura ya bandia aliyo kuwa anaitumia”
“Akhaaaa, hembu naomba viatu vyangu hapo”
Rahab alimuagiza Sa Yoon aye akafanya hivyo.
“Baby unataka kwenda wapi?”
“Ninakwenda kumuona Eddy”
“Hali yako haipo vizuri mke wangu, jaribu kutulia japo kidogo upate nguvu”
“Hapana honye mbona nina nguvu tu za kutosha”
Rahab
alizungumza huku akivaa viatu vyake. Akasimama wima, akajiweka sawa
nguo zake, akapiga hatua na kufungua mlango, akatoka na kuwaacha Sa Yoo
na raisi Praygod wakifwata kwa nyuma. Ikafika sehemu Rahab akasimama kwa
maana hakujua ni wapi alipo lazwa, ikamlazimu Sa Yoo kuwaongoza hadi
kwenye chumba alipo Eddy. Wakamkuta akisaidiwa na Phidaya kuvalishwa
shati alilo kuwa amevuliwa alipo kuwa akipatiwa huduma ya kwanza.
Rahab
akaachia tabasamu pana baada ya kumuona Eddy akiwa katika sura yake ya
halisi. Taratibu akasogea hadi kitandani, akamkumbatia Eddy kwa sekunde
kadhaa kisha akasimama wima.
“Kimetokea nini?”
“Daa sielewi yaani, nihisi kuna watu wanao nifwatilia?”
Eddy alizungumza kwa sauti iliyo poteza uchangamfu kabisa.
“Hao wana kufwatilia ni D.F.E’s”
Madam Mery alizungumza na kuwafanya watu wote ndani ya chumba hicho kumgeukia na kumtazama kwa umakini.
“Ndio nini hiyo D.F.E?”
Raisi Praygod aliuliza huku akimtumbulia macho Madam Mery
“Si
vyema kuweza kutoa ufafanuzi, hapa tulipo kwa maana sio sehemu salama
tena na tukiendelea kubaki hapa ninaamini shambulio jengine linaweza
kutokea muda wowote”
Kila
mmoja aliyesikiliza maneno ya madam Mery kwa umakini, wasiwasi ukaanza
kuwatawala kila mmoja, hususani Phidaya, ambaye kwa haraka akaanza
kuvuta kumbukumbu, siku ambayo aliweza kushika waleti(pochi) ya aliye
kuwa mume wake dokta Ranjiti na kukuta kitambulisho kilicho kuwa
kimefichwa ndani kabisa ya waleti hiyo.
Kitambulicho
hicho kiliweza kuonyesha jina sahihi la dokta Ranjiti pamoja na jina la
kundi hilo. Alipo jaribu kumuuliza dokta Ranjiti kuhusiana na
kitambulisho hicho hakupata jibu lolote la maana zaidi ya dokta Ranjiti
kumpokonya na alionekana kuwa na hasira sana.
‘Sinto hitaji uniulize swali lolote kuhusiana na D.F.E tena’
Maneno
hayo ya dokta Ranjiti, Phidaya aliweza kuyakumbuka vizuri kichwani
mwake. Phidaya akashusha pumzi nyingi huku akimtazama madam Mery usoni.
“Jamani tuondokeni”
Phidaya alizungumza huku akisimama, na kuwafanya watu wote kumshangaa.
“Ngoja nisubirie ruhusa ya madaktari mke wangu?”
“Baby hii sehemu sio salama kwa ajili yako na mimi pia?”
“Madam Phidaya kwa nini unaseme hivyo?”
Sa Yoo aliuliza huku akiwa amemkazia jicho Phidaya.
“Sina cha kujibu kwa sasa, ila Eddy kama unanipenda ninakuomba sana tutoke hapa”
“Je mwili wa Shamsa tutakwenda kuuona saa ngapi?”
Eddy aliuliza huku akishusha miguu chini kutokea kitandani.
“Hata
kesho tutakuja kuuchukua, muda umesha kwenda, na jinsi tunavyo zidi
kukaa hapa ndivyo jinsi tutakavyo zidi kupatwa na matatizo”
Phidaya
aliendelea kusisitiza kwa umakini huku mapigo ya moyo yakizidi kumuenda
kasi. Eddy akavaa viatu vyake. Alipo hakikisha kwamba yupo sawa
wakatoka kwenye chumba hicho.
***
“Yassin ni nini kimetokea mbona mbio mbio hivyo”
Khalid
alimuuliza Yassin baada ya kuingia sebleni hapo akiwa anamwagikwa na
jasho. Yassin akatazama vijana wake wapatao sita walio jiachia kwenye
masofa wakitazama mpira.
“Zimeni Tv kuna kazi nahitaji sasa hivi tukaifanye na laity tukishindwa kuifanya sasa hivi nitakosa pesa nyingi sana”
Kutokana
Yassini ndio bosi wao na ndiye anaye waongoza katika kazi zote haramu
wanazo zifanya zinazo waingizia pesa. Hapakuwa na aliye weka kipingamizi
kila mmoja akasimama kutoka kwenye sofa alilo kali. Yassin akasimama
katikati ya sable na kuwaomba wamsogelee. Akatoa simu yake mfukoni na
kuwaonyesha picha ya Eddy, ambaye alishindwa kuondoka naye hospitalini
baada ya polisi kumshinda nguvu.
“Tunatakiwa huyu kumkamata, namuhitaji mzima”
“Bosi anaitwa nani?”
“Anaitwa
Eddy, ni Mtanzania. Ila hicho si kitu cha kukiangalia kwa sasa. Kitu
ninacho kitaka ni kwenda hospitali ya Dellhan kumchukua kwani nina imani
atakuwa bado anahudimiwa kwenye hospitali hiyo”
“Sawa bosi”
“Dulla
andaa magari mawili, na kila mmoja achukue risasi za kutosha kwa maana
nilisha sababisha huko na ulinzi wa askari wa polisi upo vizuri sana”
“Bosi nina wazo?”
“Wazo gani?”
“Kama
umetoka kusababisha, basi unaonaje tukavalia mavazi ya polisi na
tukaendea pale kama polisi wa kitengo maalumu, na itatuwia urahisi
kuweza kufahamu ni wapi alipo lazwa Eddy na tukamchukua kiulaini kabisa
pasipo kutumia silaha”
“Wazo
zuri Khalid. Nguo na vitambulisho vyote view tayari. Asmah, wewe huto
valia mavazi ya askari. Valia suruali ya suti pamoja na shati yeupe. Ila
hakikisha kwamba unavalia jaketi la kuzuia risasi sawa”
“Sawa mkuuu”
“Haya
tawanyikeni dakika tano za kujiandaa. Picha ya huyu mtu nitaituma
kwenye kila simu ya mmoja wetu hakikisheni munaikariri sura yake vizuri.
Sihitaji uzembe kazini”
“Sawa mkuu”
Kila
mmoja akatawanyika na kuingia kwenye chumba chake. Huku Yassin naye
akiingia kwenye chumba chake na kuanza kujiandaa, huku sura yake
akibandika ndevu ndogo za bandia chini ya kidevu chake ili kubadilisha
muonekano wake. Pesa ambayo anaivuna kutoka D.F.E pamoja na matukio
mengi ya kiharamu. Yassin huitumia pesa hiyo kuimarisha kikosi chake
chenye vijana watano huku mwanamke akiwa mmoja na mwenye uwezo mkubwa
katika kupambana hata na wanaume kumi na anawaangusha chini ndani ya
muda mchache. Vii faa vingi anavyo vinunua ikiwemo mavazi ya polisi
pamoja na magari ya polisi, vinamsaidia sana kufanya kazi yake kwa
usahihi mkubwa pasipo kustukiwa hata na polisi wenyewe.
Ndani ya dakika tano alizo waamuru vijana wake kuweza kuzitumia, akawa
amemaliza kazi yake na kutoka chumbani kwake. Akawakuta vijana wake
wakiwa sebleni kila mmoja akiwa amesha jiandaa.
“Bosi gari zipo tayari”
“Tutagawanyika katika makundi mawili. Asmah, utakuwa name Mudathiri utakuwa na Khalid. Mulio salia mutajigawa sawa”
“Sawa mkuu”
“Kumbukeni,
tunakwenda hospitalini. Kazi inayo tupeleka pale ni mtu mmoja tu na si
mwengine. Narudia tena sinto hitaji makosa ya kizembe”
Wakatoka,
jinsi walivyo jigawa ndivyo jinsi walivyo ingia kwenye magari mawili ya
polisi ambayo wamepanga kuyatumia katika kazi iliyopo mbele yao. Safari
ikaanza kuelekea hospitalini huku kila mmoja akiwa ameishika simua yake
na kurudia kuitazama sura ya Eddy kwa mara nyingine.
***
Wakafika mapokezi, Eddy akajikuta akishangaa hali ya hapo mapokezi
kwani, ulinzi ni mkali sana na kunaonyesha kuna tukio ambalo limetoka.
“Kumetokea nini?”
Eddy aliuliza na Sa Yoo akadakia kumjibu.
“Yule jambazi aliye kuteka, alizuiliwa hapa na askari na ndio akakucha hapa baada ya kuzidiwa na yeye akaondoka”
Sa
Yoo alizungumza huku akitazama tazama eneo zima, la hapo mapokezi
ambalo ni kubwa sana. Macho yake yakautua kwa mtu aliye simama kwenye
moja ya dirisha. Moyo ukaanza kumdunda, akataka kutoka nje, ila
akasimama.
“Naomba munisubiri”
Sa Yoo alimuambia Eddy na Phidaya ambao anatembea nao karibu, huku madam Mery, raisi Praygod na Rahab tayari walisha toka.
“Unakwenda wapi?”
“Nakuja naomba munisubiri hapo nje”
Sa
Yoo hakutaka kumueleza mtu yoyote kitu anacho taka kukifanya. Eddy na
Phidaya wakatoka nje, Sa Yoo akaaza kutembea kwa mwendo wa wasi wasi
kuelekea kwenye dirisha moja la mapokezi. Kila jinsi alivyo zidi kupiga
hatua ndivyo woga ulivyo zidi kumtawala. Akamkaribia mtu aliye kusudia
kabisa kumtazama kwamba ni yeye au laa. Bila kusita akamgusa begani na
mtu huyo akageuka.
“SHAMSAAAAA…………!!?”
Sa
Yoo aliita kwa mshangao mkubwa kiasi cha kumfanya hadi nesi kushangaa.
Shamsa kumuona Sa Yoo, akajikuta akipatwa na kugugumizi.
“Sa…aaa Y…OO”
Wakatazama
kwa sekunde kadhaa huku kila mmoja akionekana kuto mtarajia kumuona
mwenzake katika sehemu hiyo hususani Sa Yoo ambaye anaamini kwamba
rafiki yake huyo amesha fariki dunia. Wakakumbatiana kwa pamoja huku
machozi yakiwamwagika.
“Nimeambiwa umekufa”
Shamsa
hakujibu kitu chochote zaidi ya kuendelea kumwagikwa na machozi. Sa Yoo
akamuachia Shamsa kidogo na kumuangalia vizuri, akahakikisha kwamba
huyu ni Shamsa, kwa maana hata nguo alizo vaa ndio nguo alizo vaa jana
usiku.
“Tuondoke rafiki yangu tunasubiriwa huko nje”
“Na nani?”
“Wewe twende, tu utawaona”
Shamsa
hakuwa na kipingamizi cha aina yoyote ziadi ya kukubaki kuondoka na Sa
Yoo. Wakatoka nje ya hospitali na kuelekea katika sehemu ambayo wapo
Eddy na wezake. Kila walivyo zidi kulikaribia eneo walipo simama Eddy na
wezake, ndivyo jinsi kila mtu alibaki akishangaa, kumuoan Sa Yoo akija
na Shamsa eneo hilo. Wakafika eneo walipo simama.
“Shamsa?”
Eddy
aliita huku macho yakimtoka, hakuamini anacho kiona mbele yake. Phidaya
akamuachia Eddy mkono na kumsogelea Shamsa, ambaye naye alibaki
akimshangaa Phidaya. Wakatazamana kwa sekunde kadhaa na kukumbatiana
huku wote wakilia kwa furaha.
“Mama nimekumsi”
“Hata mimi pia mwanangu”
Phidaya
alizungumza huku akizidi kumkumbatia Shamsa. Wakiwa katika hali bado ya
kushangaa, madam Merya akaona gari mbili za polisi zikisimama katika
maegesho yaliyopo mbele yao. Wakashuka watu sita kwenye gari mbili hizo.
Kwa haraka madam Mery akamkumbatia Eddy na kumgeuza upande mwengine na
kuanza kumnyonya denda huku viganja vyake vyote viwili vikiufunika uso
wa Eddy na kuzidi kumnyonya denda Eddy pasipio kumuhofia mtu wa aina
yoyote. Shamsa akalishuhudia tukio hilo na kumuonyesha Phidaya kitua
anacho kifanya Madam Mery, jambo lililo ipandisha hasira ya Phidaya mara
dufu na kuanza kuwafwata madama Merry na Eddy sehemu walipo simama.
0 comments:
Chapisha Maoni