“Naziomba hizi timu mbili Simba na Yanga wajue kwamba jumapili wanaenda kuonyesha vipaji vyao na walichofundishwa na makocha wao, pia wanatakiwa kutulia na sio kucheza kwa kukamiana bali soka safi kama ilivyo kwa wachezaji wa nje,” amesema Kibadeni.
Aidha Kibadeni pia amewataka viongozi wa vilabu hivyo kuweza kuwalinda wachezaji ili kutunza vipaji vyao ambavyo vitawasaidia sio kwenye soka la Simba na Yanga bali hata nje ya mipaka ya Tanzania.
Mchezo ambao unaweza kuamua mbio za ubingwa utapigwa siku ya jumapili April 29 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam. Tayari tiketi za pambano hilo zimeshaanza kuuzwa na shirikisho la soka nchini TFF.
Simba kwasasa ipo kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na alama 59 baada ya michezo 25. Yanga inashika nafasi ya pili ikiwa na alama 48 baada ya mechi 23. Baada ya pambano la jumapili Simba itabakiwa na mechi 4 huku Yanga ikibakiwa na mechi 6.
0 comments:
Chapisha Maoni