WATU
waliopembezoni ambao wamekuwa na shida kubwa ya kupata madaktari
bingwa, wataanza kupata nafuu baada ya kuanza kwa mradi wa tiba mtandao
unaoendeshwa kwa pamoja kati ya Chuo Kikuu cha Afya na
Sayansi-Muhimbili, UNESCO pamoja na wadau wengine.
Hayo
yalisemwa katika warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana
ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza. Kwa mujibu wa Mwakilishi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO)
Zulmira Rodrigues utoaji huo wa tiba mtandao kwa majaribio utaanza
mapema zaidi kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu.
Mratibu wa E-Medicine kutoka Idara ya Tiba Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Liggy Vumilia akisoma hotuba kwa
niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku
mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya
kuitekeleza inayoendelea katika ukumbi wa MUHAS jijini Dar Es Salaam.
Alikuwa
anatarajia mifumo yote kuwa tayari ifikapo Julai na hivyo kuwa na
nafasi ya kuwa katika matibabu ifikapo Oktoba. Katika warsha hiyo
aliwahimiza wataalamu kujadiliana kiundani changamoto mbalimbali na
namna ya kuweka ripoti ili kuja kusaidia wakati mradi utakapoenda
kitaifa.
Katika
warsha hiyo iliyokutanisha wataalamu mbalimbali wa tehama na madaktari
kutoka Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Dar es Salaam Katibu Mkuu Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki
Ulisubisya katika hotuba yake ya ufunguzi iliyosomwa na Dk Liggyle
Vumilia alielezea matumaini yake kuhusiana na mradi huo wa majaribio.
Aliwataka washiriki wa warsha hiyo kuona uwezekano wa kuanza mradi huo
mapema zaidi baada ya kuhakikisha kwamba dhana imekubalika na namna ya
kuitekeleza inaeleweka miongoni mwa wadau.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi-Muhimbili (MUHAS),
Prof Eligius Lyamuya alipokuwa akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki
wa warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao
na namna ya kuitekeleza inayoendelea chuoni hapo jijini Dar es Salaam.
Mradi
huo unaoanza kwa majaribio kufuatia juhudi za UNESCO zilizoanzishwa kwa
msaada wa Samsung unahusisha zaidi wagonjwa wanaoweza kufika kupata
matibabu katika kijiji cha kidigitali cha Ololosokwan na kwa kuanzia
huduma hiyo itatolewa kwa mama na mtoto na afya ya kinywa, masikio, pua
na koo (ENT), ambapo mabingwa kutoka KCMC na MUHAS wanaweza kufanya tiba
kwa kutumia mtandao.
Kliniki
ya Digitali ilizinduliwa katika kijiji cha Ololosokwan Ngorororo,
Arusha mnamo mwezi Novemba mwaka 2016. Wataalamu hao kutoka Shirika la
Afya Duniani, Mwakilishi wa Tamisemi, Wizara ya Afya, DMO wa Ngorongoro,
wataalamu kutoka KCMC na MUHAS wamekutana jana katika Kampasi ya
Muhimbili (MUHAS), ili kuangalia dhana mpya kwa ajili ya utoaji huduma
za afya kwa njia ya mtandao katika kijiji cha Wamasai, Mkoani Arusha cha
Ololosokwan.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na
Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akizungumza katika warsha ya siku
mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya
kuitekeleza inayoendelea jijini Dar Es Salaam.
Kijiji hicho tayari kina uwezo wa kupata huduma hizo.
Mradi
huo ukifanikiwa unatarajiwa kupanuliwa kwenda sehemu mbalimbali
zinazohitaji matibabu ya mabingwa lakini uwezo wa kufika huko haupo.
“Dhana hii itawezesha kuendelea na utoaji wa huduma bora za afya, zenye
ufanisi wa kitaalamu zaidi katika maeneo ya vijijini, ambayo mara nyingi
huachwa nyuma katika utoaji wa huduma hizo,” alisema Zulmira na
kuongeza kuwa dhana ya utabibu mtandao inalenga hasa kuinua utumiaji wa
teknolojia ya kidigitali ya kisasa, ambapo utekelezaji wake utakuwa
mfano elekezi wa kuboresha matumizi ya teknologia katika karne ya
ishirini na moja katika utoaji wa huduma za afya nchini na barani
Afrika.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda
akitoa neno katika warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana
ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza inayoendelea katika ukumbi wa
MUHAS jijini Dar Es Salaam.
Warsha
inayochambua dhana ya tiba mtandao ni awamu ya pili yenye kuendeleza
juhudi za kutumia uwapo wa huduma hiyo Ololosokwan kwa kuwakutanisha
wabunifu, wataalamu wa afya na wanateknolojia ili kudadavua dhana ya
utekelezaji kamilifu wa jaribio la utoaji wa huduma za afya kwa kutumia
teknolojia ya kisasa, na baadaye kuirasimisha kama mfumo wa kuboresha
afya maeneo yaliyo pembezoni ya miji na vijijini.
Katika
warsha hiyo washiriki walipata nafasi ya kushuhudia utiaji saini wa
makubaliano kati ya Unesco na MUHAS wa ushirikiano katika utekelezaji wa
dhana hiyo ya tiba mtandao. Akifafanua zaidi Dk Vumilia alisema kwamba
tiba mtandao itahusisha upasuaji mdogo ambao utafanywa na wataalamu
waliopo katika kliniki za kijiji hicho wakielekezwa na mtaalamu bingwa.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na
Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akifuatilia kwa umakini hotuba
mbalimbali zilizowasilishwa kwenye warsha hiyo.
Meneja Mradi wa Kijiji cha Kidigitali kutoka UNESCO, Tiina Neuvonen
akifafanua jambo kwenye warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia
dhana ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza inayoendelea katika Chuo
Kikuu cha Afya na Sayansi-Muhimbili (MUHAS) jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na
Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (kushoto) pamoja na Naibu Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi-Muhimbili (MUHAS), Prof Eligius
Lyamuya wakitiliana saini mkataba wa makubaliano ya kurasimisha
ushirikiano wao katika uendeshwaji wa mradi mzima wa Kijiji cha Uvumbuzi
wa Dijitali ya Afya. Wanaoshuhudia tukio hilo waliosimama ni Mratibu wa
E-Medicine kutoka Idara ya Tiba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Liggy Vumilia (kushoto) na Makamu Mkuu wa
Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda (kulia).
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na
Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu
cha Afya na Sayansi-Muhimbili (MUHAS), Prof Eligius Lyamuya na Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda
wakishuhudia Mratibu wa E-Medicine kutoka Idara ya Tiba Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Liggy Vumilia (kushoto)
akiweka saini kama shahidi wa makubaliano hayo.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na
Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu
cha Afya na Sayansi-Muhimbili (MUHAS), Prof Eligius Lyamuya
wakibadilishana hati za mkataba wa makubaliano ya kurasimisha
ushirikiano wao katika uendeshwaji wa mradi mzima wa Kijiji cha Uvumbuzi
wa Dijitali ya Afya huku tukio hilo likishuhudiwa na wataalamu kutoka
Shirika la Afya Duniani, Mwakilishi wa Tamisemi, Wizara ya Afya, DMO wa
Ngorongoro, wataalamu kutoka KCMC na MUHAS.
wataalamu
kutoka KCMC, MUHAS wadau kutoka The Africa Foundation, Aga Khan
Foundation, Ubalozi wa Uswisi, Bill & Melinda Gates Foundation,
pamoja na Maafisa wa Afya wa mikoa na wilaya za Arusha na Ngorongoro
wanaoshiriki warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya
tiba mtandao na namna ya kuitekeleza.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya (kulia) akibadilishana mawazo na Mganga Mkuu
wa Wilaya Ngorongoro, Dk. Omari Sukari wakati wa warsha ya siku mbili
ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza
inayoendelea katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi-Muhimbili
(MUHAS) jijini Dar Es Salaam. Katikati ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo
Kikuu cha Afya na Sayansi-Muhimbili (MUHAS), Prof Eligius Lyamuya. Picha ya pamoja.
0 comments:
Chapisha Maoni