Mgombea
urais wa Kenya kwa tiketi ya umoja wa vyama vya upinzani wa NASA, Raila
Odinga ameweka wazi ombi lake kwa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania,
Edward Lowassa kuhusu mchakato wa uchaguzi huo.
Amesema
kuwa Lowassa pamoja na Rais John Magufuli waliochuana kwenye uchaguzi
mkuu uliopita ni marafiki zake, na kuwaomba wote wamuunge mkono kwenye
uchaguzi huo.
Ombi
la mwanasiasa huyo mkongwe wa Kenya na Waziri wa zamani wa nchi hiyo
limekuja siku chache baada ya Lowassa kuweka wazi kuwa atamuunga mkono
Rais Uhuru Kenyatta ili aendelee kuitawala nchi hiyo.
“Mimi
na familia yangu tunamtumikia Mungu lakini vilevile kwa dhati kabisa
sisi wana Monduli tunamuunga mkono Uhuru Kenyatta kwenye mbio za Urais
nchini Kenya. Naomba nitamke wazi na dunia yote ijue kuwa sisi
tunampenda Uhuru Kenyatta naye anatupenda, kwa hiyo tunamuunga mkono kwa
kuwa tunaamini ana uwezo wa kuwaunganisha Wakenya na Watanzania,” alisema Lowassa alipotembelewa na wabunge wanawake kutoka Kenya, nyumbani kwake Monduli takribani mwezi mmoja uliopita.
Lowassa
ana ushawishi kwa kiasi fulani kwenye uchaguzi huo kwa kuwa ni kiongozi
mkuu wa Wamasai (Leigwanan) katika ukanda wote wa Afrika Mashariki.
Chama
cha Demokrasia na Maendeleo pia kimeweka wazi kuwa kitamuunga mkono
Kenyatta kwa kuwa kinaridhika na namna alivyofanya kazi hususan kuruhusu
demokrasia nchini kwake.
Hata
hivyo, msemaji wa vyama vya upinzani nchini Kenya, Philip Etale alisema
kuwa Odinga ni rafiki wa Lowassa na Magufuli na kwamba asingependa
urafiki huo upotee kwa sababu za kisiasa.
“Odinga
aliweka bayana wakati wa kampenzi za uchaguzi wa Tanzania kuwa
anawaunga mkono wote na kutaka mgombea bora ashinde. Kama ODM tunaamini
katika demokrasia na tusingependa wakati wowote ule, tupoteze marafiki
zetu kwa sababu ya siasa,” huo ulikuwa ni ujumbe wa Etale
Kenya
inatarajia kufanya uchaguzi mkuu Agosti 8 mwaka huu, uchaguzi ambao
unatajwa kuwa na ushindani mkubwa zaidi kwani katika uchaguzi uliopita,
Kenyatta na Odinga walizidiana kwa kiasi kidogo cha kura.
0 comments:
Chapisha Maoni