Takribani
watu 123 wamekufa kwa kuteketea kwa moto baada ya Lori lililokuwa
limebeba mafuta kupata ajali na kulipuka nchini Pakistan.
Taarifa
iliyotolewa na Serikali nchini humo imeeleza kuwa ajali hiyo imetokea
katika mji wa Ahmedpur Sharqia katika jimbo la Punjap ambapo watu
wengine kadhaa wameteketea vibaya, pale walipokuwa wakijaribu kuteka
mafuta kutoka katika lori hilo la mafuta.
Waliojeruhiwa wanatibiwa hospitali huku kikosi cha zima moto kipo katika eneo la ajali kikikabiliana na moto huo.
Lori
hilo la mafuta limedaiwa kuwa lilikuwa likiendeshwa kwa kasi hali
iliyosababisha kuanguka na kisha kushika moto, huku mashuhuda wakieleza
kuwa, baadhi ya watu waliofika katika eneo la ajali walikuwa wakivuta
sigara, jambo ambalo linakisiwa kuwa chanzo cha moto huo.
0 comments:
Chapisha Maoni