Tarehe
22 June 2017, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania alilipia VIUADUDU vya kutokomeza Mbu wa Malaria lita
100,000 na kuagiza vigawanywe kwenye Halmashauri zote nchini.
Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu
anapenda kuwatanganzia Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuwa
VIUADUDU hivi vitaanza kugawiwa leo (jana) kwa Halmashauri za Mikoa 14
yenye kiwango kikubwa cha Maambukizi ya Ugonjwa wa Malaria.
Mikoa
hii (na kiwango cha maambukizi ya malaria kimeonyeshwa kwenye mabano)
ni;- Kagera (41%), Geita (38%), Kigoma (38%), Ruvuma (23%), Tabora
(20%), Mtwara (20%), Mara (19%), Morogoro (14%), Shinyanga (17%), Lindi
(17%), Pwani (15%), Mwanza (15%), Katavi (14%) na Simiyu (13%),
Mikoa mingine ambayo haijatajwa itagawia Viuadudu katika Awamu ijayo.
Idadi ya Lita zitakazogawanywa kwa kila Halmashauri zilizo katika Mikoa hii tayari imeshaainishwa.
Wizara
inawakumbusha Waganga Wakuu wa Mikoa/Wilaya kufanya Upuliziaji wa
Viuadudu kwa kuzingatia Miongozo ya Wizara ya Afya. Hii itawezesha
kupata matokeo tarajiwa ya kutokomeza mbu ili kudhibiti ugonjwa wa
Malaria nchini.
Aidha,
Wizara ya Afya inapenda kumshukuru kwa dhati na kumpongeza Mhe.Rais
Dkt. Magufuli kwa kuongeza chachu katika Mapambano dhidi ya Malaria
Nchini.
Imetolewa na;
Catherine Sungura
Kaimu Msemaji- Idara Kuu Afya
26 June 2017
0 comments:
Chapisha Maoni