Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amefunguka na kusema kuwa wapinzani wa
Tanzania kama hawatabadili aina ya siasa wanazozifanya sasa basi
watapotea kwani serikali ya awamu ya tano imepata Rais ambaye hataniwi
na wala hatishiki.
Gambo
amesema kuwa wapinzani badala ya kuanza kupiga porojo zisizo na msingi,
wajipange tu kumsaidia Rais John Pombe Magufuli ili aweze kutekeleza
mambo aliyoahidi kwa Watanzania kwa miaka mitano.
"Nataka
niwaambie wanasiasa hawa wa upinzani wasipobadilisha aina ya siasa
wanayofanya kwa ninavyoiona mimi serikali ya awamu ya tano watapotea,
kwa sababu tumepata Rais ambaye hatanii.
"Unajua
wameshazoea wengine wakitishwa tishwa kidogo wanaingia mitini huyu
Magufuli akinyooka amenyooka, ananyoosha rula tu utaamua mwenyewe ukae
kushoto au kulia.
"Kwa
hiyo mimi niwashauri tu itakuwa vizuri badala ya kupiga porojo
wajipange kumsaidia Rais aweze kutekeleza mambo aliyoahidi kwa
Watanzania kwa miaka mitano" alisema Gambo
Mbali
na hilo Mkuu wa Mkoa huyo wa Arusha amesema kuwa kwa mtu yoyote ambaye
ataonekana kutaka kuikwamishan serikali basi watadili naye asubuhi,
mchana na jioni.
"Kwa
mtu yoyote ambaye ataonekana kuikwamisha serikali isitekeleze malengo
yake nataka niwahakikishie kwa uwepo wangu hapa tutahangaika naye
asubuhi, mchana na usiku kwa mbinu zote zile.
"Kama
wanataka porojo wasubiri 2020, sasa hivi kama wanataka tusaidiane
kupeleka huduma na maendeleo kwa watu, haiwezekani tukawa na serikali au
nchi ambayo kila siku ni porojo tu, kila siku siasa" alisisitiza Mrisho Gambo
0 comments:
Chapisha Maoni