Rais
John Magufuli jana alikutana na wajumbe wa kamati zilizofanya uchunguzi
wa mchanga wa madini katika makontena 277 yaliyozuiwa bandarini.
Taarifa
iliyotumwa na Kurugenzi ya Habari na Mawasiliano ya Ikulu jana umatano
ilisema Rais amewapongeza wajumbe hao kwa kazi nzuri waliyoifanya.
Kamati
hizo moja iliyoongozwa na Profesa Abdulkarim Mruma, ambaye timu yake
ilichunguza kiasi cha madini kilicho kwenye mchanga huo na ya Profesa
Nehemia Osoro iliyochunguza masuala ya kisheria kuhusu mchanga huo.
Rais
Magufuli alisema timu hiyo imefanya kazi nzuri na yenye maslahi makubwa
kwa Taifa na kwamba Serikali itahakikisha inafanyia kazi taarifa
zilizotolewa na kamati hizo.
0 comments:
Chapisha Maoni